Thursday, April 12, 2012

FILAMU ZA KANUMBA KUONESHWA DSTV MWEZI MZIMA


Kituo cha Televisheni cha Africa Magic Swahili (Dstv), kimetangaza kuomboleza msanii nguli wa filamu Tanzania, Steven Charles Kanumba, ambaye alifariki mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuonyesha filamu za msanii huyo mwezi mzima kutokana na kifo chake, ambacho kimewashtua mashabiki wa filamu Afrika.

Barbara Kambogi
Afisa Uhusiano wa Multichice Tanzania Ltd Barbara Kambogi

Kama sehemu ya kumbukumbu ya kifo chake, Dstv itakuwa ikionesha filamu zake kuanzia mwishoni mwa wiki hii kama zawadi kwa mchango wake kwenye tasnia ya filamu Afrika.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Multichoice Tanzania Ltd, Barbara Kambogi, alisema ratiba hiyo itaanza Jumamosi Aprili 14 saa 1:30 usiku, watazamaji wataanza kuangalia filamu ya Uncle JJ, Jumapili saa 2:00 usiku wataangalia filamu ya This is it (sehemu ya 1 na 2).

Kambogi alisema Aprili 21 saa 1:30 usiku watazamaji wataangali filamu ya More than Pain na Aprili 22 wataangalia Young Billionaire (sehemu ya 1 na 2), huku filamu zingine zikiendelea kuoneshwa siku zinazofuatia.


Marehemu Steven Charles KANUMBA

Mkurugenzi Mtendaji wa M-Net Africa, Biola Alabi alisema: Ni lazima tutambue nguvu ya kijana ambaye amekuwa akifanya vizuri katika tasnia hii. Kifo chake ni hasara kubwa kwa sekta ya burudani Afrika na sisi tunatoa rambirambi zetu kwa familia yake, marafiki na wapendwa wake.

Kanumba alifariki dunia siku ya Jumamosi usiku kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zilieleza.

No comments:

Post a Comment