Friday, May 25, 2012

DROGBA ASEMA CHELSEA SASA BHAAAAS..NASEPA!


Didier Drogba

Mshambuliaji Didier Drogba ataihama timu ya Chelsea ya England msimu huu wa joto, baada ya kuichezea klabu hiyo kwa muda wa miaka 8.

Mchezaji huyo wa Ivory Coast, na mwenye umri wa miaka 34, alitia kambani bao safi na la ushindi katika fainali ya mwaka huu ya Kombe la klabu Bingwa barani Ulaya dhidi ya Bayern.

Drogba atakuwa huru kujiunga na klabu yeyote ile, kwani mkataba wake na timu ya Chelsea The Blues unaelekea kumalizika.


Drogba akiwa na kombe la ligi ya mabingwa Ulaya walilolitwaa mwaka huu mbele ya Bayern Munich huko Ujerumani.

Baada ya miezi mingi ya mashabiki kutojua hatma yake, Drogba amethibitisha sasa ataondoka Stamford Bridge.

"Nilitaka kukomesha hali hii ya shaka na kuthibitisha kwamba ninaondoka Chelsea", alielezea Drogba katika tovuti ya Chelsea.

"Umekuwa ni uamuzi mgumu sana kwangu, lakini ni fahari kwangu kwa ufanisi tulioweza kupata, lakini wakati umewadia kwa changamoto mpya", alielezea.

Aliongezea: "Kama timu, tumefanikiwa katika mengi, na tukishinda vikombe muhimu."

"Ningelipenda kuitumia nafasi hii kuwashukuru wote katika klabu, hasa Roman Abramovich na wachezaji wenzangu."



Tatizo la mkataba wa Drogba ulianza msimu uliopita, wakati klabu ilipokataa kumuongezea miaka miwili zaidi katika mkataba wake.

Wasiwasi wa mashabiki ulizidi wiki chache zilizopita, iwapo Drogba ataendelea kuichezea Chelsea, hasa baada ya timu yake kuibuka mshindi katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya Liverpool, na pia alipofunga bao la kusawazisha Jumamosi, na vilevile kufunga goli la ushindi wakati wa mikwaju ya penalti baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Bayern.

No comments:

Post a Comment