Saturday, June 9, 2012

UFUNGUZI EURO 2012 POLAND YABANWA MBAVU,URUSI YAANZA UNONO

Source News Feed: EMEA Picture Service ,Germany Picture Service

Referee Carlos Velasco Carballo of Spain (2nd L) shows a red card to Poland's goalkeeper Wojciech Szczesny (2nd R) during their Group A Euro 2012 soccer match against Greece at the National stadium in Warsaw, June 8, 2012. REUTERS/Pawel Ulatowski (POLAND - Tags: SPORT SOCCER)
Mlinda mlango wa Poland Szczeny akilimwa kadi nyekundu

Mwachemwache ya UEFA EURO 2012 ilinza jana huku ikishuhudiwa matukio chungu nzima katika mecho zote mbili zilizosakatwa. Katika mechi za kundi A, Poland ilitekwa nayo Urusi ikang'ara.      
Timu inayopigiwa upatu katika kundi A Urusi iliiangamiza Jamhuri ya Czech magoli manne kwa moja, nayo Ugiriki ikaharibu karamu ya wenyeji wa dimba hilo Poland kwa kulazimisha sare ya goli moja kwa moja wakati timu zote mbili zikimaliza mchuano na wachezaji kumi kila upande.
 
Mlinda mlango wa Pooland Szczeny akicheza undava langoni mwake

Nahodha wa Urusi Andrei Arshavin alionyesha mchezo mzuri wakati timu yake ikionyesha umahiri wa mbinu ya mashambulizi mjini Wroklaw, Poland, na kuizika timu ya Czech.
Warusi sasa watacheza na Poland ambao walikuwa na mwanzo mzuri dhidi ya mabingwa wa UEFA EURO 2004 Ugiriki wakati mshambuliaji wao Robert Lewandoski alipotikisa wavu mapema lakini Wagiriki walijizatiti na hata wakashindwa kufunga penalti katika mchuano huo wa kusisimua.

Kuanza kwa mechi uwanjani kulisaidia kuondoa hofu dhidi ya tatizo la ubaguzi wa rangi katika kinyang'anyiro hicho, ambacho Poland inaandaa kwa pamoja na Ukraine na ndicho kikubwa zaidi cha aina yake mashariki mwa Ulaya tangu kuanguka kwa utawala wa kikomunisti.
Mambo yangekuwa mabaya zaidi kwa timu ya nyumbani lakini kipa aliyeingia kama nguvu mpya Przemyslaw Tyton aliokoa penalti zikiwa zimesalia dakika 20 mchuano kukamilika.
Mlinda lango nambari moja wa Poland Wojciech Szczesny alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumtendea madhambi Dimitris Salpingidis katika eneo la hatari lakini mkwaju hafifu wake nahodha wa Ugiriki Giorgos Karagounis ukapanguliwa na Tyton.

Urusi yaiduwaza Jamhuri ya Czech
Katika mchuano wa pili Urusi ilifungua ukurasa wa magoli mawili ya kwanza yaliyofungwa na Alan Dzagoyev baada ya dakika 15 naye Roman Shirokov akaona wavu katika dakika ya 24 kabla ya Vaclav Pilar kuwafungia goli moja Waczech katika kipindi cha pili.
Dzagoyev aliongeza lake la pili katika dakika ya 79 naye nguvu mpya Roman Pavyluchenko akasukuma wavuni kombora zikiwa zimesalia dakika nane mechi kukamilika.


Mlinda mlango wa Jamhuri ya Czech Peter Cech akichumpa bila mafanikio wakati Alan wa Urusi akitupia kambani goli la kwanza.

Yalaaaaah kaniumizaaa!! ndivyo anavyosema Konstantin wa Urusi alipochezewa undava na Jaroslav Plasil wa Czech

Mhhh mambo magumu..ndivyo anavyosema mlinda mlango wa Jamhuri ya Czech Peter Cech

Nahodha wa Urusi Andrei Arshavin alionesha uwezo binafsi

Poland na Ukraine wanataraji kuwa dimba hilo litauonyesha ulimwengu mafanikio yaliyopatikana tangu ukuta wa Berlin ulipoangushwa mnamo mwaka wa 1989 na Muungano wa Usovieti kuvunjika miaka miwili baadaye, huku Ukraine ikitaka fainali hizo ziisaidie kutangamana na mataifa ya magharibi.
Hata hivyo nchi hizo mbili zinakumbwa na mgogoro kuhusu ubaguzi wa rangi, huku nchikadhaa zikipanga kususia dimba hilo kutokana na namna Ukraine inavyomnyanyasa kiongozi wa upinzani aliye gerezani Yulia Tymoshenko, katika kesi ambayo nchi za magharibi zinasema ilichochewa kisiasa.
Mechi zitakazochezwa nchini Ukraine zitaanza leo Jumamosi wakati Uholanzi itakapocheza na Denmark nayo Ujerumani kugaragazana na Ureno katika kundi gumu la B.
Kocha wa kikosi cha Ujerumani Joachim Löw huenda yuko tayari kukichagua kikosi chake kwa kuzingatia wachezaji kadhaa wa Bayern munich ambao walishindwa na Borussia Dortmund katika taji la Bundesliga kabla ya kushindwa na Chelsea kwa penalti katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Wachezaji hao ni kama vile Thomas Müller, Mario Gomez, Philip Lahm , Jerome Boateng, Manuel Neuer na Bastian Schweinsteiger…
Poland na Ugiriki

Urusi na Jamhuri ya Czech

No comments:

Post a Comment