Tuesday, August 7, 2012

NDUGAI AFUNGUKA WABUNGE HUINGIA MJENGONI WAMEPIGA "VYOMBO"

Wakati Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania likiwa bado kwenye kashfa ya rushwa mapya yameibuka kama "movie" vile tunatoa picha hii tunaweka picha ile na uzuri wa Watanzania huwa hatumalizii picha tunaishia katikati na hii ni nafuu kwa Mafisadi.

Naibu Spika na mbunge wa Kongwa,Dodoma(CCM) amefunguka na kutoa shutuma nzito kwa waheshimiwa kuwa na tabia ya kuingia mjengoni na kuhudhuria vikao vya Bunge wakiwa wamepiga "vyombo" kama vile Sigara kubwa(Bangi),Maji ya Mende(Bia) na nyeupe(madawa ya kulevya),
Amewashutumu Baadhi ya waheshimiwa ambao huonekana kupitia kamera za Mjengoni wakiwa wamelala na kusingizia uchovu.

Hivi ndivyo Mh Job Ndugai alivyofunguka “Kuna wabunge ninavyohisi wanaingia bungeni wakiwa wamevuta sigara fulani kubwa, kulamba vitu fulani au hata kupata bia mbili tatu,” alisema Ndugai akihojiwa jana asubuhi katika kipindi cha medani za siasa na uchumi cha Star tv.
Ndugai alifunguka kuwa madudu hayo hubainika mida ya kuanzia mchana na akalaumu kuwa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa pindi "kipande" kinapobainika kimeingia mjengoni huku kikiwa kimepiga "vyombo". “Wabunge ni watu kama watu wengine, wana tabia kama walivyo wanadamu wengine, wapo ambao kwa namna ninavyohisi wanaingia bungeni hasa vikao vya kuanzia mchana wakiwa wamepiga bia,” alisisitiza
Ndugai

No comments:

Post a Comment