Thursday, August 30, 2012

REAL MADRID YATIA KIBINDONI KOMBE LA SUPERCOPA


Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia na kombe la SUPERCOPA
 
Timu ya soka ya Real Madrid ya Uhispania imeanza kuweka kabatini makombe ya nchini Uhispania baada ya kuichabanga Barcelona magoli 2-1 katika dimba lao la nyumbani,Santiago Bernerbeu ambao pia ni mji mkuu wa Uhispania.

Ushindi wa Real Madrid wa mabao 2-1 ulifanya matokeo ya jumla kuwa 4-4 baada ya mechi ya kwanza iliyopigwa Nou Camp Barcelona kuilaza Rea Madrid kwa kamba 3-2, Na sasa Real Madrid imepata ushindi kutokana na kufanikiwa kutupia kambani magoli mengi ugenini.
Hi-res-150649730_crop_exact
Kazi moja tu Pique na Pedro

Katika mchezo huo wa jana Barcelona iliyoonekana kutokuwa imara sehemu ya Ulinzi na kuwaruhusu Real Madrid kutupia kambani goli 2 za fastafasta, Real Madrid walianza mchezo huo kama kwamba waliambiwa waingie kuharibu mipango na utulivu wa mtindo wa uchezaji wa Barcelona na walifanikiwa kwa 100%, na kwa kutumia udhaifu wa Safu ya Ulinzi ya Barcelona iliyokuwa chini ya Pique na Mascherano mafundi Christiano Ronaldo na Higuain walifanikiwa kuipatia Real Madrid magoli muhimu katika mchezo huo ingawa Higuain mchezo ulionekana kutokumkubali kwa sana.

Makosa ya kizembe yaliyofanywa na Adriano ya kupewa kadi nyekundu yaliigharimu Barcelona kucheza pungufu kwa dakika za mwisho za kipindi cha kwanza na zote za kipindi cha pili.

Real walikuwa wa kwanza kutupia kambani kupitia Higuian katika dakika ya 11 na dakika 9 baadae Christiano Ronaldo aliipatia Real goli la pili kabla ya Leonel Messi kutupia kambani kwa "free kick" ya umbali wa mita 30 dakika chache kabla ya kwenda mapumziko.

Christiano Ronaldo akijiandaa kuachia "fataki" na kufunga goli la pili.
 
Christiano Ronaldo akishangilia baada ya kutupia kambani goli la pili dhidi ya Barcelona

Higuain Akishangilia goli la kwanza


Luka Modric akiangalia kombe la kwanza kulitwaa akiwa Real Madrid limeshikiliwa na Pepe na Ronaldo.

Hi-res-150521084_crop_exact
Mambo magumu..nisepe mie" ndivyo anavyoonekana kuwaza Leonel Messi

Katika mchezo wa jana timu zote ziliingiza majembe waliyoyasajili kutoka Ligi kuu ya Uingereza, Barcelona wakimuingiza Alexander Song aliesajiliwa kutoka Arsenal na Real Madrid wakimuingiza Luca Modric aliesajiliwa kutoka Tottenham Hotspurs zote za Uingereza.

No comments:

Post a Comment