Thursday, January 17, 2013

MAN U,ARSENAL ZATAKATA KOMBE LA FA

Vigogo wa ligi kuu ya Uingereza Man United na Arsenal jana zimefanikiwa kupenya raundi ya nne ya Kombe la FA baada ya kupata ushindi katika mechi zao za jana Arsenal ikiizabua timu iliyoonesha upinzani mzuri kuanzia mechi ya awali ya Swansea kwa goli 1-0 huku wenzao Man United wakiichabanga Westham kwa bao 1-0.

Arsenal waliizabua Swansea kwa bao 1-0 katika dimba lao la Emirates mpambano ukishuhudiwa na watazamaji wapatao 58,359. Umati huo ulishuhudia mpambano mkali ambao ulitawaliwa zaidi na timu ya Arsenal huku wakikosa magoli mengi katika mpambano huo. Baada ya kosakosa nyingi katika dakika ya 85 wakati jua likielekea magharibi ya roho sio mwingine bali ni kipenzi cha waingereza Jack Wilshere aliewainua vitini mashabiki wa Arsenal kwa kutupia kambani goli pekee na la ushindi kwa mkwaju mkali uliomshinda Vorm mlinda mlango wa Swansea.
Mpaka mwamuzi wa mchezo huo Clattenburg anapuliza kipyenga cha mwisho matokeo yalikuwa Arsenal 1-0 Swansea. Kwa matokeo hayo Arsenal wameitupa nje ya kombe la FA timu ngumu ya Swansea na kupenya raundi ya nne.

Wilshere akifumua nduki iliyotinga moja kwa moja kambani kuandika bao la Arsenal


Wilshere akilipuka kwa furaha baada ya kufunga goli dhidi ya Swansea

Patashika langoni mwa Swansea

Vikosi vilikuwa;

Arsenal

  • 01 Szczesny
  • 03 Sagna
  • 04 Mertesacker
  • 05 Vermaelen
  • 28 Gibbs
  • 02 Diaby (Ramsey - 82' )
  • 10 Wilshere
  • 14 Walcott
  • 19 Cazorla
  • 22 Coquelin
  • 12 Giroud

Substitutes

  • 24 Mannone
  • 11 Santos
  • 25 Jenkinson
  • 15 Oxlade-Chamberlain
  • 16 Ramsey
  • 23 Arshavin
  • 09 Podolski

Swansea City

  • 01 Vorm
  • 02 Bartley
  • 04 Chico
  • 21 Tiendalli
  • 07 Britton
  • 12 Dyer
  • 15 Routledge
  • 20 De Guzman (Ki Sung-Yeung - 60' )
  • 26 Agustien (Pablo - 59' )
  • 29 Richards
  • 10 Graham (Michu - 71' )

Substitutes

  • 25 Tremmel
  • 16 Monk
  • 33 Davies
  • 09 Michu
  • 11 Pablo
  • 24 Ki Sung-Yeung
  • 17 Shechter

Man United nao walifanikiwa kuivurumisha nje ya kombe la FA timu ya Westham baada ya kuibanjua kwa goli 1-0 katika dimba la Old Trafford huku mtanange huo ukihudhuriwa na mashabiki wapatao 71,081.  Alikuwa ni Wayne Rooney akiripoti rasmi baada ya kuwa nje ya dimba kwa wiki nne alipotupia kamabni bao la pekee na la ushindi katika dakika ya 8 tu ya mchezo baada ya kupata pande murua kutoka kwa Chicharito.


Rooney akifunga goli dhidi ya Westham

Rooney akipiga penati ambayo iliota mbawa

Carrick akijaribu kuwatoka mabeki wa Westham

Manchester United

  • 13 Lindegaard
  • 02 Rafael
  • 04 Jones
  • 12 Smalling
  • 28 Buttner
  • 07 Valencia
  • 08 Anderson (Carrick - 67' )
  • 11 Giggs
  • 17 Nani (Scholes - 77' Booked )
  • 10 Rooney
  • 14 Hernandez

Substitutes

  • 40 Amos
  • 05 Ferdinand
  • 16 Carrick
  • 22 Scholes
  • 26 Kagawa
  • 19 Welbeck
  • 20 Van Persie

West Ham United

  • 22 Jaaskelainen
  • 02 Reid
  • 05 Tomkins
  • 27 Spence Booked
  • 33 Potts
  • 14 Taylor
  • 21 Diame (Collison - 65' )
  • 23 Diarra
  • 32 O'Neil
  • 09 Cole (Nolan - 65' Booked )
  • 12 Vaz Te (Lee - 78' )

Substitutes

  • 30 Spiegel
  • 20 Demel
  • 04 Nolan
  • 07 Jarvis
  • 10 Collison
  • 43 Lletget
  • 47 Lee
ARSENAL 1-0 SWANSEA

MAN U 1-0 WESTHAM U

No comments:

Post a Comment