Monday, September 23, 2013

BREAKING NEWZ!!!!!!!! WESTGATE NCHINI KENYA KIMENUKA JENGO LALIPULIWA

Huu ni muhtasari uliotolewa na BBC Yaliyojiri Huko Westagate
15:20 Polisi waonekana wakikimbia huku na kule katika harakati zao hizo dhidi ya Al Shabaab

14:56 Mkuu wa majeshi Meja Jenerali Julius Karangi amesema magaidi hao wanaweza kujisalimisha ikiwa wanataka kwa sababu jeshi litakabiliana nao vilivyo. Pia amesema kuwa Kenya inakabiliana na magaidi wa kimataifa

14:35 Ole Lenku anasema kuwa hali ingali tete lakini vikosi vya usalama vya Kenya vinakaribia kuwazingira magaidi hao...Hadi kufika sasa watu 62 wamefariki na wengine zaidi ya 175 kujeruhiwa. Pia ameongeza kuwa magaiodi wote ni wanaume, kutokana na taarifa za awali kuwa magaidi hao walikuwa wanaongozwa na mwanamke

14:30 Ole Lenku anasema kuwa wanajeshi kumi wamejeruhiwa na wanapokea matibabu. Pia mateka karibu wote wameweza kuokolewa. Ole Lenku pia amesema kuwa wameweza kuwaua magaidi wawili

14:28 Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku anasema kuwa moshi ulitokana na moto uliosababishwa na magaidi wlaioko ndani ya jengo hilo kujaribu kusambaratisha juhudi za wanajeshi wa Kenya dhidi yao

14:03 Mkuu wa polisi David Kimaiyo asema kuwa vikosi vya usalama vinakaribia kudhibiti jengo hilo lote na vimeingia ndani kabisa ya jengo hilo kiasi cha kuwaokoa baadhi ya mateka
14:00 PM: Milipuko zaidi yasikika katika jengo hilo

13:54: Mwandishi wa BBCIdriss Situmaaliye katika eneo la Westgate anasema duru zinaarifu kuwa vikosi vya usalama vya Kenya vinasema kuwa ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia ndani kabisa ya jengo hilo
13:52 PM Magari ya Ambulance yaobnekana yakienda katika eneo la shambulizi pamoja na magari ya zima moto. Vikosi vya usalama vinawataka watu kuondoka karibu na eneo la operesheni hiyo ili kuwawezesha kufanya kazi yao

13:49 pm: Moshi mkubwa mweusi waonekana ukitoka juu ka juu katika jengo hilo haijulikani nini kilichosababisha
13:19 pm Moshi mkubwa unaonekana ukitoka katika jengo la Westgate ambako wapiganaji wa Al Shabaab wanawazuilia mateka wakenya ambao idadi yao haijulikani

13:12 PM Viongozi wa kidini watoa taarifa kulaana kitendo cha Al Shabaab
12:30 PM: Milipuko zaidi na milio ya risasi imesikika katika jengo la Westgate huku vikosi vya usalama vikifanya jitahada za misho kuwa
 Heavy smoke rises from the Westgate Mall in Nairobi, Kenya
Westgate ikiwaka moto
 
Wanausalama wakikabiliana na Magaidi

Mwamanchi akijaribu kujinusuru

Polisi wakiwanusuru wananchi

Wanausalama wakiokoa wananchi


Maiti Westage






 
 
Majeruhi wakisaidiwa





Masikini mtoto wa watu katika taharuki
















No comments:

Post a Comment