Thursday, April 3, 2014

UEFA PSG YAICHARAZA CHELSEA, REAL MADRID YAITANDIKA DORTMUND

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ametangaza wazi kuudhika sana na safu yake butu ya mashambulizi.
Mourinho aliyasema hayo punde baada ya kushuhudia PSG ya Ufaransa ikiititima 'the blues' mabao matatu kwa moja katika mkondo wa kwanzawa mechi ya robo fainali ya kombe la mabingwa Barani Ulaya.
 
Wayaaaaaaaa
 
Laveziiiii wayaaaaaaaaaaaa

Wenyeji PSG waliweka wazi ari yao ya kusonga mbele baada ya dakika pekee kupitia kwa Ezequiel Lavezzi .
Vijana wa Jose Mourinho nao wakajifurukuta na kufanya mashambulizi ambayo yalizaa penalti baada ya Oscar kuchezewa visivyo katika eneo la lango.
Eden Hazard akafanya mambo kuwa 1-1 katika dakika ya 27.
Nipe nikupe iliendelea hadi kipindi cha pili PSG walipofaidika na bao la kujifunga mwenyewe la David Luiz kunako dakika ya 61.
Hawakukomea hapo ,Javier Pastore alihakikisha Chelsea itakuwa na mlima wa kupanda nyumbani kwao Stamford Bridge katika mkondo wa pili mbali na kuibua kumbukumbu za mwaka wa 2004 timu hizo
mbili ziliposajili matokeo sawia na hayo PSG ilipokuwa mbioni kucheza katika fainali ya kombe la mabingwa .
Aidha mechi ya kwanza kwa mkufunzi Jose Mourinho alipochukua hatamu Stamford bridge ilikuwa dhidi ya Paris St-Germain mwezi September 2004.
Wakati huo The Blues waliwatandika PSG 3-0 John Terry na Didier Drogba wakiandikisha majina yao katika orodha ya wafungaji.
 
Ibrahimovic akiwanjonjofya wachezaji wa Chelsea
 
Mwamuzi na wachezaji wa PSG wakimuangalia Zlatan Ibrahimovic baada ya kutengenezwa na Ramires.

Hatoki mtu hapa.....Ibrahimovic akioneshana udamwidambwi na David Luiz

ThiagoSilva na Torres hakatwi mtu hapa

We bwege tuuu......mwamuzi wa pembeni akiwahi mpambano kati ya Cavani na Luiz

''Mhhh hali tete'' Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akiduwazwa na matokeo.

REAL MADRID Vs DORTMUND

 Vigogo wa ligi kuu ya Uhispania ambao wamekuwa wakisuasua katika mechi za la liga Real Madrid, wamedhibitisha udedea wao katika ligi ya mabingwa bara Uropa baada ya kuiadhibu vikali Borussia Dortmund ya Ujerumani katika mkono wa kwanza wa robo fainali ya mchuano huo iliyochezwa Santiago Bernabeu.
Real iliilaza Borussia Dortmund mabao matatu kwa Ubuyu .
Real ilidhihirisha nia yao mapema Gareth Bale alipofuma bao la kwanza kunako dakika ya tatu ya mechi hiyo.
 
 
Bale akitupia kambani bao la kwanza
 
CR9 akishangilia baada ya kutengeneza kamba ya pili

Isco alitikisa wavu na bao la pili katika dakika ya 27, huku bao la tatu likifungwa naye Cristiano Ronaldo dakika ya 57 kipindi cha pili.
Bao hilo la mchezaji bora msimu wa 2013 lilimsaidia Ronaldo kusawazisha rekodi ya idadi kubwa ya mabao kuwahi kufungwa kwa msimu mmoja wa dimba hilo la mabingwa barani Uropa.
Bao la Ronaldo lilikuwa la 14 katika mechi nane za ligi ya mabingwa , sawia na rekodi iliyowekwa na Lionel Messi katika mwaka wa 2011-2012.
Kwa upande wao Dortmund ambao walishindwa katika fainali mwaka uliopita na Bayern Munich watajilaumu wenyewe kwa kutotumia vyema fursa 12 walizopata kushambulia lango la Real.
Hata hivyo vijana hao wa Jurgen Klopp walidhihirisha wazi bila nyota wao Robert Lewandowski safu yao ya ushambulizi ni butu.
Wajerumani hao wanajuma moja tu kusahihisha makosa walioyafanya jana kabla ya mechi ya marudio ambayo imeratibiwa kuchezwa tarehe 8 Aprili huko ujerumani.


Namie nimooooooooooooo...Isco akishangilia goli pamoja na Bale
 
Safi sana dogo, CR9 akimpongeza Isco

Msifikiri nimefurahi naumiaaaaaaaaa...kocha wa Borussia Dortmund
 
PSG 3-1 CHELSEA
 
REAL MADRID 3-0 DORTMUND

No comments:

Post a Comment