Utafiti mpya umeonyesha kwamba wanawake walio na uraibu wa kuvuta sigara wako katika hatari ya kupata maradhi ya moyo zaidi kuliko wanaume walio na uraibu huo.
Utafiti ulioendeshwa miongoni mwa zaidi ya watu milioni mbili umepata wanawake wako kwenye hatari ya maradhi ya moyo kwa asili mia 25 wakati wanapotumia tumbako.
Sababu za matokeo haya hazijatolowa japo watafiti kutoka Marekani wamesema wanawake wako kwenye hatari kubwa ya kuvuta kemikali zenye simu kutoka kwa sigara ikilinganishwa na wanaume.
Hali hiyo wameongeza imejitokeza katika idadi ya wanawake wanaopata saratani ya mapafu ikilinganishwa na wanaume wanaovuta sigara.
Ramani ya Tanzania
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika linaloshughulikia maslahi ya watoto la UNICEF karibu theluthi moja ya watoto wa kike nchini Tanzania wanakabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia na kuingiliwa bila hiari kabla hawajatimia umri wa miaka 18.
Shirika hilo linasema kuwa watoto wa kiume idadi yao inafika asili mia 13.4.Kinachotumika sana katika unyanyasaji huu ni kuwatomasa watoto ambako baadae hufuatiwa na jaribio lakutaka kuwaingilia.
"Tanzania ndio nchi ya kwanza kuwa jasiri kufichua tatizo hilo linalowakabili watoto wa kike na wakiume" alisema Andy brooks afisa wa UNICEF.
Uchunguzi huu pia uligundua kuwa wale ambao wamejihusisha na mapenzi kabla ya kutimia umri wa miaka 18, asili mia 29.1 ya watoto wa kike na asili mia 17.5 ya wale wa kiume wamesema kuwa mara ya kwanza wao kujihusisha na ngono haikuwa kwa hiari yao.
Unicef inasema hii ina maana walilazimishwa ama kushawishiwa kujihusisha na ngono.
Waziri wa Elimu wa Tanzania Shukuru Kawambwa amesema kuwa serikali imejitolea kukomesha unyanyasaji wa kijinsia na kuingiliwa watoto.
Bw Brooks amesema uchunguzi sawa na huo utafanywa nchini Kenya, Rwanda, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kusini.

