Monday, May 30, 2011

HATIMAE WAFUNGUA UKWELI WAO KUHUSU BARCELONA

Hakuna kitu kizuri kama mtu kusema kweli na kukubali mazuri ya mwenzake, mchezaji wa Man United Patrice Evra amefunguka na kukiri kuwa Barcelona wamekuwa wazuri zaidi ya miaka minne iliyopita.
Patrice Evra.
"Lazima uwapongeze Barcelona, hata kama nachezea Man na tunataka kuwa bora duniani..lakini Barcelona ni bora zaidi" anasema Evra. "Tunafahamiana lakini Barcelona wanafahamiana zaidi, kila mara Messi anajua Xavi atakua pale na Pedro atakuwa pale au Iniesta..ilikuwa mechi ngumu Barca walimiliki mpira vizuri sana" anamalizia Evra.
Kocha na meneja wa Man United Sir Alex Furgerson amefunguka na kusema kuwa Wamefungwa na timu bora japokuwa walitegemea kufanya vizuri mwisho wa siku wameambulia kipigo. "Tulitegemea kufanya vizuri lakini mwisho wa siku tukaambulia kipigo kutoka kwa timu bora" alisema Fargie.

No comments:

Post a Comment