Monday, May 30, 2011

NANI KAMA MESSI.


Kwa jinsi nilivyoingalia Barcelona ni timu nzuri ambayo huwezi kuibeza hata kama una mapenzi na timu pinzani, Meneja wa Man United Sir Alex Furgerson na mchezaji wake Evra wamefunguka na kukiri hilo nami ninaungana nao kuwa Barcelona wamekuwa wazuri ndani ya miaka minne. katika kikosi cha Barcelona hakuna mchezaji wa kubeza na hili nalitamka kwani nimepata kuongea na Javier Mascherano kabla ya fainali ya jumamosi na alisema kuwa hatojisikia vibaya kama hatoanza katika mechi hiyo kwani Barcelona ina wachezaji wengi mahiri na yeye anajisijia fahari kuwa miongoni mwa kikosi hicho bora duniani. Hivyo naamini kila mchezaji ana uwezo binafsi ndani ya Barca lakini nadiriki kusema Leonnel Messi kuwa mchezaji bora wa fainali ile amestahili na ataendelea kuwa bora. staili ya uchezaji wa Messi ni kitu cha kushangaza unaweza kusema viatu vyake na mpira vinavutana ni hali ya uchezaji isiyoelezeka yaani kama uchawi vile lakini ukweli ni kwamba kipaji na mazoezi ya kujituma ndio siri ya hayo yote.

No comments:

Post a Comment