Wednesday, May 25, 2011

PIQUE AKUMBUKA MACHOZI MAN UNITED.

Pique akumbuka alivyomwaga chozi Man United


BEKI wa Barcelona, Gerard Pique, akumbushia enzi zile alipokuwa Man United na kufunguka kwamba aliwahi kumwaga machozi wakati alipokuwa akikipiga Manchester United – lakini, Jumamosi hii Mhispania huyo atakutana na United katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, itakayofanyika kwenye dimba la Wembley, jijini London.
                                     Gerlard PiqueAkiwa ndani ya jezi za Mashetani Wekundu hao wa Old Trafford, Pique anashukuru kwa sababu aliweza kutwaa mataji tisa na Kombe la Dunia.
Man United imebaki kuwa sehemu muhimu katika maisha yake ya soka, licha ya kwamba hakucheza mechi nyingi katika kikosi hicho cha Sir Alex Ferguson, na kudai kwamba yeye binafsi ana deni kubwa la kumshukuru Mskochi huyo.
“Nilikwenda England nikiwa na miaka 17 na mambo yalikuwa magumu sana,” alisema Pique.
“Nilizoea kuwa kiwanjani katika kila mechi, lakini kwa bahati mbaya siku nyingine za mechi mimi nilikuwa nikiachwa nyumbani.
“Iliniumiza sana, na niliona sikustahili yale. Lakini, wakati ule sikuwa sawa na nilipokuwa Manchester United.
“Nilijifunza jinsi ya kukabiliana na nyakati ngumu. Nilimpigia simu mama yangu mzazi na kumweleza yote baada ya kutokwa na machozi sana.”
Pique Jumamosi hii atakuwamo ndani ya dimba wakati Barca itakapokipiga na Man United katika fainali hiyo ya Mabingwa Ulaya katika dimba la Wimbley nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment