Tuesday, May 24, 2011

TANZANIA KUJITANGAZA LIGI ZA ULAYA.

Sh5bil kuitangaza Tanzania Ligi za Ulaya Send to a friend
Monday, 23 May 2011 20:51
                                                Rais wa Tanzania, Mh Jakaya Mrisho Kikwete.
SERIKALI imejipanga kuitangaza sekta ya utalii hapa nchini kwa kupitia michezo na kwa sasa imeweka mkakati wa kutoa matangazo ya utalii katika viwanja vinane vya soka ulimwenguni vinavyotumiwa na timu za ligi kubwa duniani.

Jumla ya sh5billioni zitatumika kwa zoezi hilo kuitangaza Tanzania katika ligi za England, EPL, Hispania, La Liga, Italia, Seria A, Ufaransa, Lique 1 na Ujerumani ya Bundesliga.Mbali na viwanja hivyo pia nafasi hiyo itatumika kutangana za Tanzania na utalii katika nchi za Ureno, Uholanzi pamoja na Uturuki.

No comments:

Post a Comment