Tuesday, May 24, 2011

Kipa Mkenya asaini Simba miaka 2 Send to a friend
Sunday, 22 May 2011 20:37

Willis Ochieng

BAADA ya mazungumzo ya kina na uongozi wa klabu ya Simba, hatimaye kipa wa kimataifa wa Kenya, Willis Ochieng amesaini rasmi mkataba wa miaka miwili wa kuichezea timu hiyo.Ochieng ambaye awali alikuwa anacheza soka ya kulipwa katika klabu ya IFK Mariehamn ya Finland kabla ya kumalizika mkataba wake Novemba mwaka, jana alitua nchini Alhamisi ya wiki iliyopita kwa ajili ya kukamilisha taratibu za usajili ili aweze kuichezea Simba katika msimu ujao wa ligi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Akizungumza na Mwananchi jana akiwa njiani kurudi nchini Kenya, Ochieng alisema kuwa mpango wake wa kujiunga na Simba umekamilika na tayari amesaini mkataba wa miaka miwili."Nashukuru kilichonileta nimekamilisha, nimezungumza vizuri na watu wa Simba na nimesaini kucheza katika klabu yao kwa mkataba wa miaka miwili,"alisema Ochieng.

Alisema,"Kimsingi nilipenda kucheza hapa kwa sababu mazingira ya kufanya kazi Kenya na Tanzania yanafanana na hata urafiki wa watu wake ni wa karibu sana hivyo ni dhahiri ninaweza kufanya vizuri na kuisaidia Simba kufikia malengo yake."

Ochieng alisema anaelekea nyumbani kwao Kenya kwa ajili ya kuwaaga ndugu na jamaa na kwamba atarejea nchini baada ya wiki moja kujiunga rasmi na wenzake.

"Nilikuja kwa ajili ya kuweka mambo sawa na hilo limemalizika, naelekea nyumbani kuaga ndugu na jamaa na nitarejea baada ya wiki moja kuanza kazi rasmi,"alisema Ochieng.

Kipa huyo ameshazichezea klabu za Mumias Sugar ya nchini Kenya pamoja na Free State ya Afrika Kusini, alisema kuwa atalazimika kufanya juhudi zaidi ili aweze kupata nafasi ya kuwa kipa namba moja.

"Mimi sijafanya mazungumzo ya kuja kuwa kipa namba moja hilo litatokana na juhudi nitalazimika kuzifanya na si rahisi kama watu wanavyoongeza, Simba ina makipa wazuri kama Juma Kaseja ni mmoja wao hivyo ni dhahiri ushindani utakuwepo,"alisema Ochieng.Wakati huo huo; Jessca Nangawe anaripoti kuwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi anatua leo akitokea nchini kwake Afrika Kusini alipokuwa akifanya majiribio na klabu ya Kaizer Chief

No comments:

Post a Comment