Wednesday, May 25, 2011

ZUMA KUTEMBELEA LIBYA KWA MAZUNGUMZO NA GADDAFI

Moshi ukifuka nyuma ya mitikufuatia shambulio la anga katika eneo la Tajura
km 30 mashariki mwa Tripoli wakati majeshi ya NATO yaliposhambulia Tripolitarehe 24 mei 2011 katika harakati za kumng'oa Gaddafi.
Rais Jacob Zuma wa Afrika ya kusini anategemewa kutembelea Libya wiki ijayo, ambapo inaripotiwa kuwa safari hiyo ni maalum kwa ajili ya mazungumzo na kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi,ambapo radio moja nchini Afrika ya Kusini Radio 702 inaripoti kuwa mazungumzo hayo yatahusu juu ya mikakati ya Gaddafi kuondoka nchini Libya. Zuma atadhuru Tripoli kwa mazungumzo na kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi tarehe 30 mei 2011. Zuma anadhuru Libya akiwa kama kiongozi wa juu wa umoja wa Afrika katika kutatua mgogoro wa Libya, Zuma anadhuru Libya huku mwishoni mwa wiki Afrika ya kusini iliilalamikia Libya kwa kumtendea ndivyo sivyo mpiga picha wa Afrika kusini ambaye hivi sasa inaaminika kuwa amekwishakufa baada ya kupigwa risasi na askari wa Gaddafi.

No comments:

Post a Comment