Tuesday, June 7, 2011

BURRESS AMALIZA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI.

Hatimaye mchezaji mashuhuri wa NEW YORK GIANTS siku ya jumatatu tarehe 6 mida ya saa tatu asubuhi aliachiliwa huru kutoka gerezani ikiwa ni miezi mitatu kabla ya kifungo chake kukamilika kutokana na kuonesha tabia njema akiwa gerezani na kurudi nyumbani kwake Florida baada ya kutumikia kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kukutwa na silaha, ambapo siku ya tukio novemba 2008 akiwa katika klabu ya usiku jijini  New York kwa bahati mbaya risasi aliyoiweka kiunoni ilifyatuka na kumpiga katika mguu na kusababisha kukamatwa kwake na silaha kinyume na sheria.

                        Plaxico Burress akitoka Gerezani.

Plaxico Burress akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka gerezani.

Plaxico Burress akiwa amembeba mwanae Elijah Burress baada ya kutoka gerezani.

        Plaxico Burress uwanjani kabla ya kukamatwa kwake.


Akiwa amevalia mavazi meusi,sweater jeusi,t-shirt nyeupe na pale chini ametupia sneakers nyeusi akiwa peke yake kutoka gerezani na kuangaza huku na huko na kumuona meneja wake Drew Rosenhaus na kumrukia kwa furaha."Napenda kumshukuru mungu kwa kunipa moja ya mitihani maishani mwangu" alisema burress, "Napenda niwashukuru wote kwa maombi na maneno ya kunitia nguvu nikiwa gerezani" aliongeza Burress. Burress ambaye mwezi wa nane anatimiza miaka 34 alijitupia ndani ya Range Rover na kuungana na mkewe tayari kwenda nyumbani kufungua ukurasa mpya wa maisha baada ya kifungo.
Burress alitoka gerezani akiwa amevalia kofia ya Philadelphia Phillies na inasemekana kuna uwezekano mkubwa akarudi kuichezea tena na wakati huohuo kuna uwezekano wa timu ya New York Jets wakamchukua ili kuziba pengo la Braylon Edwards aliyestaafu.

No comments:

Post a Comment