Friday, June 24, 2011

CLICHY ANATAKA KWENDA LIVERPOOL

Gael Clichy
Beki wa Arsenal Gael Clichy binafsi amesema anahitaji kwenda Liverpool. Akiwa amebakiza miezi 12 mkataba wake na Arsenal uishe mchezaji huyo anataka kuishawishi Asenal kufanya mazungumzo na Liverpool ambayo imetoa ofa ya paundi za Uingereza milioni 5, Maamuzi hayo ni ya kushangaza kidogo kwani tayari klabu ya AS Roma ya Italy tayari imeshatangaza dau la paundi za Uingereza milioni 7 ikiwa ni milioni 2 zaidi ya dau la Liverpool lakini Clichy inaonekana anafurahia zaidi kuendelea kubaki Uingereza.

No comments:

Post a Comment