Thursday, June 16, 2011

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA.

Leo ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, Siku hii barani Afrika inaadhimishwa huku kukiwa na changamoto nyingi zinazoikabili jamii nzima ya Afrika kuhusiana na malezi ya watoto. Watoto Afrika wanakabiliwa na changamoto za maisha duni ya jamii kubwa barani Afrika ambapo katika nchi nyingi za kiafrika inaaminika kuwa familia nyingi zinaishi maisha ya taabu ambapo matumizi ya familia kwa siku yanasadikika kuwa ni chini ya dola moja ya kimarekani. Kutokana na jamii kubwa kuwa na maisha ya hali ya chini inapelekea malezi ya watoto nayo kuwa duni,watoto wanakosa haki za msingi kutokana na familia zao ama wazazi kutokuwa na uwezo wa kuwatekelezea haki hizo ambazo ni pamoja na haki ya kusoma, chakula, malazi,michezo na haki nyinginezo.

Watoto wana haki ya kupata elimu.

Siku hadi siku wimbi la watoto wa mitaani limezidi kuongezeka kutokana na ukweli kuwa maisha yanazidi kupanda kadri siku zinavyozidi kwenda na familia nyingi kujikuta kusambaratika kutokana na kutokuwa na uwezo wa kukaa pamoja na kupata mahitaji ya kila siku.

Watoto wana haki ya kupata chakula bora.

Leo ikiwa ni siku ya mtoto wa Afrika hatuna budi kutafuta mbinu za kukabiliana na matatizo yanayowakabili watoto, tuangalie ni jinsi gani tunaweza kuboresha mazingira yao ya kusomea yaani shule, pia tuweze kuangalia jinsi gani tutawatoa watoto waliopo mitaani ambapo hapa Tanzania inasadikika watoto wa mitaani ni wengi sana hasa katika mikoa ya Dar es salaam, Dodoma,Mbeya,Singida na Kilimanjaro. Viwanja vya kuchezea watoto visimilikiwe na watu kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki yao ya msingi, Kwa pamoja tuwe na wito unapomuona mtoto a mwenzio basi umuone na kumthamini kama mtoto wako wa kumzaa hapo ndio tunaweza kuwalea na kuwatunza katika maadili yaliyo mazuri.
Watoto wana haki ya kucheza.

Watoto wana haki ya kulala mahala safi na salama.





No comments:

Post a Comment