Monday, August 29, 2011

CHELSEA YAIADHIBU NORWICH CITY 3-0

Juan Mata
Juan Mata

Juan Mata katika mechi yake ya kwanza katika uwanja wa Chelsea wa Stamford Bridge, aliweza kufunga bao lake la kwanza akiichezea timu yake mpya, na kuiwezesha kusonga hadi kuongoza ligi kuu ya Premier, angalau kwa muda mfupi, baada ya kuifunga Norwich magoli 3-1.

Liverpool baadaye ilijipenyeza hadi nafasi ya kwanza, kwa kupata ushindi kama huohuo, ilipocheza katika uwanja wa nyumbani wa Anfield dhidi ya Bolton na kuizaba magoli 3-1.

Hata hivyo, licha ya kupata ushindi, mashabiki wengi wanafikiria kwamba Chelsea haikucheza kama ilivyotazamiwa.

Chelsea walikuwa wa kwanza kupata bao, kupitia mchezaji Jose Bosingwa, lakini Norwich wakasawazisha kupitia mchezaji Grant Holt.

Frank Lampard alitia wavuni mkwaju wa penalti na kuongeza mabao hadi 2-1, baada ya kipa John Ruddy kumwangusha Ramires, akihisi mchezaji huyo wa Chelsea alikuwa anajiandaa kufunga.

Mata aliiandikishia Chelsea ushindi, lakini raha ya ushindi huo kugubikwa na kutojua hali ya Didier Drogba ni vipi, baada ya kujeruhiwa kichwa.

Kipa Ruddy alikuwa anajaribu kuondosha mpira alipompiga ngumi ya uso Drogba.

Katika mechi nyingine, Aston Villa na Wolves walishindwa kufungana, na mechi kwisha 0-0.

Matokeo yalikuwa ni kama hayo pia katika mechi kati ya Swansea na Sunderland.

Everton iliwafunga Blackburn goli 1-0.

Wigan nayo iliwafunga QPR magoli 2-0.

Kuhusiana na Liverpool kuishinda Bolton na kuwa kileleni, meneja Kenny Dalglish ameisifu timu yake ya Liverpool, akisema walionyesha wazi kwamba waling'ara katika uwanja wa Anfield.

Kenny Dalglish
Meneja wa Liverpool amewasifu wachezaji wake kwa kuwa kileleni katika ligi kuu ya Premier

"Ilikuwa ni burudani kutazama walivyocheza," alielezea baadaye, kufuatia mabao kutoka kwa Jordan Henderson, Charlie Adam na Martin Skrtel.

Meneja wa Bolton Owen Coyle alikiri kwamba Liverpool walistahili ushindi wao wa magoli 3-1 lakini akaongezea: "Tulijiharibia wenyewe mwanzo wa kipindi cha pili kwa kuwaruhusu kutufunga magoli mawili zaidi."

Bao la Ivan Klasnic ambalo lilipatikana katika dakika za mwishomwisho katika mechi halikuwapa faraja yoyote Bolton.

No comments:

Post a Comment