Friday, August 19, 2011

JUKWAA LAANGUKA WAKATI WA TAMASHA LA MUZIKI NA KUUA

Nchini Ubelgiji jukwaa limeanguka na kuua watu kadhaa, Jukwaa hilo lilianguka katka tamasha la muziki linalojulikana kama Pukkelpop Music Festival jijini Hasselt, watu wanne wameripotiwa mapema kufariki dunia katika tukio hilo.

Belgium-Pukkelpop
Watu wakiwa wamepigwa na butwaa katika tukio hilo.

Msanii Cullen Omori amekaririwa mapema leo hii akisema "Ndio kwanza tulikuwa tumemaliza kuimba wimbo wetu wa kwanza katika nyimbo zetu hapa Pukkelpop, ndipo jukwaa na hema vikaanza kutingishika na tukafikiri labda ni kimbunga tu kinapita, ndipo nikaamrisha tuendelee na wimbo wa pili ndipo meneja wa msafara alisikika akipiga yowe kuwa tuteremke kutoka jukwaani, mara ghafla upande mmoja ukaanguka futi moja kwenda chini, tukafikiri kuwa ni jukwaa tu ndio limeanguka na sio hema ghafla vilio na kelele vilitosha kutueleza kilichotokea, lakini mpaka wanauja waokoaji na kututaarifu kuwa kuna watu waliopoteza maisha wapatao wanne na kadhaa wamejeruhiwa, huruma na mawazo yetu yakawa kwa wale waliowapoteza wapendwa wao katika janga hili."

Tazama jinsi ilivyokuwa

No comments:

Post a Comment