Monday, August 15, 2011

STOKE CITY YAIKOMALIA CHELSEA

Stoke imeweza kuizuia Chelsea katika mechi iliyokuwa na matokeo ya kukatisha tamaa ya bila kufungana ambapo walinzi wa Stoke walifanikiwa kuwavurugia mipango yao washambuliaji wa Chelsea.
Hekaheka Stoke na Chelsea
Torres akijaribu kufunga bila mafanikio

Wakati wa kipindi cha kwanza Fernando Torres akionekana kupania kuitafutia bao Chelsea, Stoke walikuwa wakitumia zaidi mipira ya pembeni kuanzishia mashambulio.
Chelsea walijirekebisha kipindi cha pili na kucheza vizuri wakati John Obi Mikel alikaribia kupachika bao kwa mkwaju wake wa mbali na baadae Nicolas Anelka mkwaju wake ukapaa juu katika lango la Stoke.
Chelsea walidai wapatiwe mkwaju wa penalti wakati Marc Wilson alipomtegea Frank Lampard.
Matokeo ya mechi hiyo yameacha maswali kwa meneja wa Chelsea boss Andre Villas-Boas kutokana na uamuzi wake wa kumuanzisha Torres badala ya Didier Drogba.

No comments:

Post a Comment