Monday, October 24, 2011

JOKATE MWEGELO APEWA SHAVU SASA NI MTANGAZAJI CHANNEL O
















Jokate kushoto akiwa na watangazaji wenzake wapya wa Channel O.

DStv’s Channel O Africa imemteua mwigizaji na mwanamitindo Jokate Mwegelo kuwa mmoja wa watangazaji wake wapya sita.
Kituo cha televisheni cha Channel O kilifanya usaili nchi mbalimbali na Tanzania ni Jokate aliyefanikiwa kuibuka kidedea.
Washindi wengine wanatoka katika nchi za Nigeria, Uganda, Kenya, Ghana na Afrika kusini.

Kuanzia sasa utakuwa ukimuona Jokate katika mitaa mbalimbali akiwa na kamera na mic za channel O kwa kuwa hiyo ndiyo ajira yake mpya jijini. “Ukikaa karibu na Jokate, umekaa karibu na Channel O”.

Vigezo vilivyotumika kumpata mwakilishi huyo nchini ni kujua vizuri historia ya muziki wa nyumbani na vitu vingine mbalimbali kwani ndivyo atakavyotakiwa kuripoti.

No comments:

Post a Comment