Friday, November 11, 2011

11-11-2011



Ni vyema ukahakikisha siku ya leo unaandika tarehe ya leo kwa mkono wako, Leo ni tarehe 11-11-2011.
Hizi namba zinavyonana hasa wale tunaopenda kuandika kwa kifupi,mfano leo tutaiandika hivi 11-11-11. Kutokana na ufupisho huo ukiutazama kwa makini ni kama unaona milango mitatu,sasa basi kwa mtazamo huo na kwa jinsi namba za tarehe hii zinavyofanana ni ukweli kuwa hazitatokea tena katika siku za maisha yetu yote.
Milango mitatu kwa mtazamo maana yake ni hii,

Mlango wa kwanza, Huu ni kwa wale ambao hawana imani ya dini yeyote,huku hawapo na kule hawapo na hata hapo walipo hawapo,mlango huu wa kwanza kutoka kushoto unaashiria tarehe na kama tunavyofahamu tarehe inadumu kwa masaa 24 tu halafu inabadilika..tafakari

Mlango wa Pili,yaani katikati ambao unawakilisha mwezi, Huu ni kwa wale ambao imani zao ni mguu nje mguu ndani yaani vuguvugu. Kama tunavyojua mwezi ni siku 30 ama 31 halafu unabadilika.....Tafakari

Mlango wa Tatu,yaani mlango wa kulia huu ni maalum kwa wale ambao imani zao zipo sawia na matakwa ya Mungu wao,Na upande huu unawakilisha mwaka na kama tunavyojua mwaka una siku 365 na 1/4  halafu unabadilika unakuja mwaka mwingine..tafakari.

Fanya uamuzi sasa aidha uwe baridi,vuguvugu au baridi.


Kwahiyo basi ni vizuri ukatenga muda wako japo kwenye kipande cha karatasi ukaiandika tarehe ya leo na kwa imani yako takatifu utakuwa umejitendea haki kwani tarehe hii ni muhimu katika kujipima imani yako imelala upande gani..Naamini kwa kusoma habari hii tayari kwa muda huu umekuwa karibu na mungu wako. 11-11-11.

No comments:

Post a Comment