Tuesday, November 1, 2011

MATONYA ANAMILIKI HOTELI YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 150


Seif Shabaan a.k.a MATONYA

Mwanamuziki Nguli katika sanaa ya Tanzania ya muziki aina ya bongo flavour Seif Shaaban maarufu kwa jina la Matonya hakika anaweza kuwa mfano wa miongoni mwa wasanii wenye mafanikio hapa Tanzania "BONGO".
Matonya aliyeanza muziki mwaka 2000 na wimbo wake wa kwanza kuuachia ulikuwa ni uaminifu mwaka 2001.
Matonya ambaye mbali na muziki ni mfanyabiashara ya magari kutoka nje amefanikiwa kwa kiasi kikubwa na hivi sasa anamiliki hoteli yenye thamani ya shilingi milioni 150 za kitanzania.
Hoteli hiyo ipo Tanga mjini mtaa wa White Rose na inatarajiwa kufunguliwa miezi michache ijayo. hongera sana Tonya boy..

No comments:

Post a Comment