Tuesday, November 15, 2011

MCHEZAJI MWINGINE AFIA UWANJANI NI WA NIGERIA

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Nigeria Bobsam Elejiko, alianguka uwanjani na kufariki dunia wakati akiichezea timu yake ya Ubelgiji ya Merksem SC siku ya Jumapili.
Bobsam Elejiko afariki dunia uwanjani
Bobsam Elejiko afariki dunia uwanjani

Beki huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa akicheza mechi dhidi ya FC Kaart wakati alipoanguka na kupoteza fahamu.


Elejiko akitolewa nje ya uwanja kwa machela baada ya kuanguka na kufa papo hapo

Majaribio ya kuuzindua moyo wake yalishindikana na sababu za kifo chake hazijaelezwa mara moja.

Taarifa iliyotolewa na klabu ya Merksem imesema:"Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo kilichotokea ghafla cha Bobsam Elejiko." Mechi hiyo ilisimamishwa baada ya kifo cha Elejiko.


Jopo la madaktari likijitahidi kumzindua Elijiko bila mafanikio

"Alianguka na kufa hapo hapo uwanjani na rambirambi zetu tunazitoa kwa familia yake na marafiki."
Elejiko alishawahi kuchezea klabu za Westerlo na Antwerp

No comments:

Post a Comment