Rais wa Syria Bashar Al-Asaad
Marekani imepongeza shinikizo za karibuni kutoka jamii ya kimataifa dhidi ya kiongozi wa Syria Bashar Al Assad kumtaka aachie madaraka. Msemaji wa Ikulu ya Marekani amesema rais Assad anazidi kutengwa na dunia hususan baada ya Syria kusimamishwa uanachama wa Muungano wa nchi za Kiarabu.
Mfalme wa Jordan, King Abdullah
Mapema jana Mfalme wa Abdullah wa Jordan alimwomba kiongozi huyo wa Syria kuachia ngazi. Lakini msemaji wa serikali ya Syria amesema mfalme huyo anafaa kusaidia kutatua mizozo ya kanda hiyo na siyo kuigawanya.
Duru kutoka kwa makundi ya kutetea haki za bandamu ambazo bado hazijathibitishwa zinasema mejeshi yaliyoasi wamekabiliana na jeshi tiifu kwa serikali katika mji wa kusini mwa nchi. Katika makabiliano hayo raia sita waliuawa na idadi sawa ya jeshi kufa.
Umoja wa Mataifa unasema takriban watu elfu tatu wameangamia katika machafuko ya kisiasa yanayoendelea Syria, licha ya shinikizo za kimataifa kwa taifa hilo kuzuia maafa ya raia.
Waziri wa mambo ya nje wa Syria Wallid Muallem
Katika mkutano na waandishi wa habari, waziri wa mambo ya nje wa Syria Wallid Muallem alikiri kwamba rabsha za wikendi iliyopita, wakati wafuasi wa Rais Bashar Al Assad walipozilenga afisi za kibalozi za Saudi Arabia, Uturuki na Ufaransa na Qatar mjini Damascus, hazitashuhudiwa tena. Nchi hizi zimekuwa mstari wa mbele kulaani utawala wa Syria kwa kutumia nguvu kupita kiasi nguvu dhidi ya raia wanaompinga Rais Assad.
Jumuiya ya nchi za kiarabu imetoa pendekezo la kutuma ujumbe maalua wakiwemo waandishi wa habari, waangalizi wa kijeshi na wale wa haki za kibinadamu kuchunguza hali ilivyo nchini Syria.
No comments:
Post a Comment