Wednesday, January 25, 2012

Gabon ngoma inogile kombe la mataifa ya Afrika

Waandalizi wenza wa Kombe la Mataifa ya Afrika, Gabon wameanza vizuri mchezo wao wa kwanza katika kundi C walipoifunga Niger mabao 2-0 mjini Libreville.

Gabon vs Niger
Wagabon walikuwa wakiwachagiza tangu mwanzoni mwa mchezo kutafuta bao ambalo halikuja hadi kipindi cha pili zikiwa zimesalia dakika thelathini kabla mpira haujamalizika.
Nyota wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang aliunganisha krosi kutoka kwa Stephane Nguema na kufunga bao la kwanza kwa kichwa.
Nguema aliandika bao la pili kwa Gabon.
Baada ya waandaaji wenzao Equatorial Guinea kushinda mchezo wa ufunguzi kwa kuilaza Libya 1-0 siku ya Jumamosi, Gabon walikuwa katika changamoto kubwa na wao kufanya kile wenzao walichokifanya.

Tunisia vc Morocco

Nayo Tunisia walitumia makosa ya wachezaji wa Morocco waliocheza kwa kiwango cha chini kwa kuwalaza majirani zao wa Afrika Kaskazini kwa mabao 2-1 katika mchezo wa ufunguzi wa kundi C.
Khaled Korbi alikuwa wa kwanza kuipatia bao Tunisia kwa mkwaju wa adhabu ya moja kwa moja hadi ndani ya nyavu za Morocco.
Youssef Msakni aliyeingia mchezaji wa akiba aliiongezea Tunisia bao la pili kwa mkwaju mkali bada ya kuwazunguka na kuwatoka walinzi wa Morocco kwa chenga za kuvutia, kabla ya nahodha wa Houcine Kharjah kupata bao la kufutia machozi.
Morocco walipoteza nafasi nyingi za kupata mabao lakini Tunisia walistahili kushinda baada ya kuonesha kandanda ya kuvutia.

No comments:

Post a Comment