Wednesday, January 25, 2012

Real Madrid kufuta uteja kwa Barcelona leo?


Kocha wa Barca Pep Guardiola


Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho

REAL Madrid wanatakiwa kusahau mbinu yao ya kujilinda na kucheza kwa kushambulia dhidi ya Barcelona kwenye mchezo wa pili wa robo fainali ya Kombe la Mfalme leo.Kocha wa Madrid, Jose Mourinho amekuwa kwenye wakati mgumu kwa mbinu yake hiyo iliyosababisha wakafungwa 2-1 wiki iliyopita na Barcelona, Mreno huyo alirudia tena Jumapili waliposhinda 4-1 dhidi ya Athletic Bilbao.
Ushindi huo ulionyesha ubora wa kushambulia wa Madrid wakiongoza ligi na kuicha Barcelona kwa pointi tano baada ya kufunga mabao 67 katika mechi 19 walizocheza hadi sasa.Bado Mourinho hajaomba radhi mbinu za Madrid katika mchezo wa kwanza, kitendo kilichowaudhi hata mashabiki wa kocha huyo pamoja na vyombo vya habari vya Madrid.
Jumapili gazeti la Marca liliandika kuwa kumekuwa na mvutono kwenye vyumba vya kubadilisha wakati Mourinho alipokuwa akitangaza kikosi cha kucheza dhidi ya Bilbao kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu hiyo ni mara ya kwanza kutokea kwa kocha huyo tangu alipotua hapo 2010.
“Chochote kilichosema kuhusu mgawanyiko au madai ya kugombana ni uongo,” Sergio Ramos aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, siku moja baada kutokea mabishano kati ya beki huyo wa Madrid na Mourinho. “Hili ni kundi bora wenye umoja, bila ya kujali nini kimesemwa.”Safu ya ushambuliaji wa Madrid itaimarika kama mshambuliaji wa Argentina, Angel di Maria atakuwa amepona majeruhi yake.
Beki Pepe haijulikana kama atacheza baada ya kuwekwa benchi kwenye mchezo dhidi ya Bilbao kufutia kitendo chake cha kumchezea vibaya Lionel Messi kwenye mchezo wa kwanza.Madrid imeshinda mechi moja kati ya 13 walizocheza dhidi ya Barcelona hiyo ilikuwa kwenye fainali ya Kombe la Mfalme mwezi Aprili na wamefungwa mechi tisa.
Barcelona itashuka dimbani ikiwa na rekodi ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Malaga, huku Messi akiweka rekodi ya kufunga mara 10 katika ligi mabao matatu 'hat trick' kwa mabingwa hao wa Ulaya.
Messi kwa sasa amefunga mabao 36 kwenye mashindano yote msimu huu, huku Alexis Sanchez ameweza kuendana na mchezo wa mabingwa hao na tayari mshambuliaji huto wa Chile ameshafunga mabao tatu katika mechi nne zilizopita.
“Wanaongoza ligi, wanaweza kufuzu kwa nusu fainali ya Copa na wapo kwenye raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa. Kwa mtazamo wa nje ni vigumu kujua kama wana matatizo au hapana,” alisema kiungo wa Barcelona, Andres Iniesta juzi.
Pia, Mirandes inahitaji kuifunga Espanyol ili kuwa timu ya kwanza ya daraja la tatu kufika nusu fainali tangu ilipofanya hivyo Fugueres mwaka 2002. Mirandes ipo nyuma kwa 3-2 itashuka kwenye uwanja wake Manispalaha ya Andova wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 6,000.
Wakati huo huo, Valencia na Athletic Bilbao wenye wanajivunia ushindi wao mkubwa waliopata kwenye mechi za kwanza.Valencia watakuwa wageni wa Levante kesho wakiwa mbele kwa 4-1 nao Bilbao walioshinda 2-0 wataivaa Mallorca leo.

No comments:

Post a Comment