Thursday, March 22, 2012

ARSENAL YAICHAPA EVERTON,VERMAELEN NI NOUMER!


Arteta na Van Pesie wakishangilia goli lililofungwa na Vermaelen(5)

Theo Walcott akipunguzwa makali na Leighton Baines wa Everton

Timu ya soka ya Arsenal jana tarehe 21 machi 2012 waliutumia vizuri uwanja wake wa Emirates uliopo jijini London kwa kuichabanga Everton bao moja kwa ubuyu(1-0).
Katika meshi hiyo ndani ya dimba la Emirates ilihudhuriwa na watu 30,330 na mchezo huo ulichezeshwa na Mason.
Arsenal ambao wanaonekana kuwa fit kwa kila mechi kipindi hiki walicheza soka la kuvutia kama kawaida yao na sio mwingine aliepeleka msiba Everton bali ni Beki anaeongoza kwa kutupia kambani Thomas Vermaelen aliposukumiza mpira wa kichwa wavuni katika dakika ya 7 ya mchezo.
Mpaka mapumziko Arsenal walitoka kifua mbele kwa goli moja la kuongoza,Kipindi cha pili kilianza kwa soka la kuvutia huku Gunners wakijaribu kuongeza bao na Everton nao wakifanya jitihada kutafuta bao japo la kufutia machozi bila mafanikio.
Japo washambuliaji wa Arsenal kama Ramsey,Rosicky na Van Persie walijaribu kuchafua hali ya hewa golini mwa Everton lakini ngome ya Everton iliyoongozwa na Baines akisaidiana na Heitinga na Distin ilikaa vyema na mpaka dakika 90 zinakamilika Arsenal ndiyo iliyoibuka mshindi.

Timu:
ARSENAL; Szczesny, Sagna, Vermaelen, Koscielny, Gibbs, Walcott, Arteta, Song, Ramsey, Rosicky, van Persie

EVERTON; Howard, Hibbert, Heitinga, Distin, Baines, Pienaar, Fellaini, Osman, Drenthe, Cahill, Jelavic.

No comments:

Post a Comment