Thursday, March 22, 2012

MANCHESTER CITY YAIBOFOA CHELSEA 2-1


Golikipa wa Man City Joe Hart akichumpa bila mafanikio kuokoa mpira uliopigwa na Garry Cahill ukielekea kambani.

Aguero akitupia kambani kwa mkwaju wa penati na kuisawazishia Man City

Nasri akitupia kambani na kuandika bao la pili na la ushindi kwa Man City,Cech hoooooi

Manchester City imeendeleza kampeni zake za kuusaka ubingwa wa Ligi kuu ya Uingereza pale ilipoichabanga timu ngumu ya Chelsea kwa kamba 2-1 mchezo uliopigwa katika dimba la Etihad jijini Manchester.Mchezo ulipigwa jana tarehe 21 march 2012 ukichezeshwa na refa mahiri Dean.

MAN C 2-1 CHELSEA
Katika kipute hiko iliwachukua takriban dakika 60 mashabiki waliohudhuria mtanange huo kushangilia bao na bao hilo likitiwa kambani na Garry Cahill na kuifanya Chelsea kuongoza mchezo huo uliokuwa wa kawaida tofauti na ulivyotegemewa na wengi.
Mbwembwe za mashabiki na wachezaji wa Chelsea za kuongoza zilikomeshwa katika dakika ya 78 pale refa Dean alipoizawadia mkwaju wa penati Man City na bila ajizi wala kokoro mkwaju huo ulitiwa kambani na Sergio Aguero na kubadilisha taswira ya mchezo na kusomeka 1-1.
Zikiwa zimesalia dakika 5 ili kila mshabiki alielipia mechi hiyo kuhesabu maumivu kwa kuona mchezo wa sare Vijana wa Manchini walikaza na kufanikiwa kuwanyanyua vitini mashabiki wa Man City huku wakiwaonesha milango ya kuondokea wale wa Chelsea, kwa goli kali na la kuvutia lililotupiwa kambani na Mshambuliaji mzuri wa sura na uchezaji Samir Nasri katika dakika ya 85.
Bao hilo la Nasri lilionekana kuwachanganya Chelsea hasa kocha wao wa kuunga unga De Matteo na kushindwa kukaa kwenye benchi akiwahimiza kina Drogba kufanya mambo bila mafanikio yeyote na mpaka dakika 90 zinakwisha ni Man City ndio walioibuka kidedea na kuwaacha Chelsea walikwa wamelowa ndembendembe kama laki si pesa.
Vikosi vilikuwa hivi;

MAN CITY; Hart, Zabaleta, Richards, Toure, Clichy, Silva, Toure Yaya, De Jong, Nasri, Aguero, Balotelli

CHELSEA; Cech, Ivanovic, Luiz, Cahill, Cole, Mikel, Meireles, Ramires, Lampard, Mata, Torres

No comments:

Post a Comment