Monday, March 26, 2012

MAAMUZI YA TFF KUPENDELEA VILABU VIKUBWA YANAUA SOKA LETU(kusimamisha adhabu za wachezaji wa Yanga)

TFF kupitia kamati ya Usuluhishi na Nidhamu(kamati ya Tibaigana) imesimamisha adhabu walizopewa wachezaji mabondia wa Yanga, kwa madai kuwa kamati ya ligi ya TFF haina mamlaka ya kutoa maamuzi yaliyotolewa. maswali yanakuja;
1-nani alipeleka mashitaka kwenye kamati hiyo?
2-walikuwa wapi muda wote huo kusema kuwa kamati ile haina mamlaka?
3-Kamati ile ilitumia vielelezo vipi kutoa adhabu kwa wachezaji mpaka kamati ya usuluhishi na nidhamu iseme Tff hawajapeleka vielelezo?
4-Wamesimamisha adhabu zilizotolewa na kamati ya ligi na adhabu alizotoa refa zinaendelea,sasa mchezaji Mwasika aliyempa refa ngumi ya uso hakupewa hata kadi ya njano inakuwaje?
5-Kuna wachezaji kama Cannavaro wameshatumikia adhabu ya kadi aliyopewa je maamuzi mengine yatakayotolewa na kamati ya usuluhishi na nidhamu hayatamuathiri?
5-Kamati ya ligi imetoa adhabu ngapi na Hazikupingwa na kamati ya nidhamu na usuluhishi(kamati ya Tibaigana)?


Ninaamini kamati ya Ligi ya TFF ina watu makini na ni viongozi makini na hata aliyepeleka mashitaka kwenye kamati hiyo aliamini inaweza kufanya maamuzi na ndio maana kamati ikafanya kazi yake sasa hii kamati ya Tibaigana iliyotengua maamuzi hayo ninaamini walikuwa na taarifa ya maaamuzi ya kamati ya Ligi iweje wakakaa kimya mpaka sasa wakati wachezaji wameshatumikia adhabu waseme kamati haina hadhi ya kutoa maamuzi?

Naomba niwe muwazi katika hili sidhani kama adhabu hizo wangekuwa wamepewa wachezaji wa Oljoro au Coastal Union kamati ya Tibaigana ingehangaika kuzisimamisha na kutumia muda kukaa vikao vingine, ikumbukwe hapo gharama zimetumika kuita waandishi wa habari pale habari maelezo watu wakaacha kazi zao wakakaa kusikiliza maamuzi ya kamati ya Ligi na watu wakalipana posho na waandishi wakatumia gharama kuandika habari ya adhabu za wachezaji hao na wananchi wakatumia pesa zao kununua magazeti kupata habari hizo halafu mwisho wa siku pamoja na usumbufu na gharama zote hizo anatokea mtu na kusema maamuzi yametolewa na kamati isiyokuwa na mamlaka,najiuliza mlikuwa wapi muda wote huo kama sio hii kamati ya Tibaigana kufanya kazi kwa maslahi ya timu fulani?

Hakika soka letu kwa utendaji wa kubabaisha kama huu litaendelea kudidimia wadau tujiandae kupinga adhabu itakayotolewa na kamati ya usuluhishi na nidhamu ambayo kwa hili hatuna imani nayo.

No comments:

Post a Comment