Monday, March 26, 2012

SIMBA YAFANZA KWELI YAWARUDISHA ES SETIF ALGERIA VICHWA CHINI


Wachezaji wakisalimiana kabla ya mpambano huo kuanza

Timu ya soka ya Simba ya jijini Dar es salaam imefanya kweli katika kombe la shirikisho kwa kuifunga timu ngumu ya ES Setif kutoka algeria katika mechi ya awali iliyopigwa katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es salaam kwa kuibuka na ushindi mnono wa bao 2-0.
Katika mchezo huo uliokuwa na upinzani mkali Waarabu walionekana kucheza mchezo wa kujihami huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini ngome ya Simba iliyoongozwa na Kelvin Yondan sambamba na Nyosso wakisaidiwa vyema zaidi na beki za kushoto na kulia smbso ni Shomari Kapombe na Maftah na pale katika milingoti miwili alikuwepo Tanzania one Juma K Juma.
Katika mpambano huo uliohudhuriwa na mashabiki 41,000 na zaidi Mpaka mapumziko hakukuwa na timu iliyoweza kuliona lango la mwenzake.

Kosakosa langoni mwa Setif

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi zaidi hasa kwa timu ya Simba kana kwamba kocha alishawasoma Setif mchezo wao wa kutegea na kufanya mashambulizi ya kushtukiza kwa kucheza pasi fupifupi katika nusu yao na wanapofika nusu ya pili kuelekea langoni mwa Simba walikuwa wakipiga pasi ndefu.Simba kipindi hiki walikuja na kasi na kufanya mashambulizi mengi katika lango la Setif na tabu ililetwa langoni mwa Setif kwa juhudi kubwa za viungo waliocheza kwa ushirikiano mzuri kati ya Kazimoto,Machaku na Haruna Moshi"Boban" ambapo kwa kiasi kikubwa Simba wana kila sababu kujivunia beki ya kulia na kushoto yaani Maftah na Kapombe waliofanya kazi kubwa kupandisha mashambulizi mbele na hii ilileta nafuu kwa washambuliaji Okwi,Sunzu na Boban.
Felix Sunzu alitumika vizuri kuwaweka mabeki wa Setif katika wasiwasi na kujikuta wakimkaba kwa jihadi na kutoa mianya kwa Okwi na Boban kuleta mashambulizi langoni mwao.
Baada ya dakika 75 za ukame wa magoli ndipo jitihada za wachezaji wa Simba zilipozaa matunda wakati Mshambuliaji wa Kimataifa toka Uganda Emmanuel Okwi alipotupia kambani bao la kwanza na kuamsha shamrashamra kwa wapenzi wa Simba na hata wale wasio na mapenzi na Simba waliohudhuria katika dimba kuu la Taifa.









Mashabiki wa Yanga waliokuwa wakiibeza Simba lakini mwisho wa siku walitoka uwanjani na chupi yao mkononi na aibu tele

Goli la Okwi liliamsha morari kwa wachezaji wa Simba na Setif walioonekana kama wamezinduka toka usingizini na kuanza kusaka bao la kusawazisha lakini jitihada zao ziligonga mwamba pale Mshambuliaji mwingine wa Simba toka Zambia Felix Sunzu alipotupia kambani goli la pili katika dakika ya 80 baada ya kipa wa Setif kutema kombora la Machaku.

No comments:

Post a Comment