Thursday, May 31, 2012

BALOTELLI ATOA ONYO EURO, UKILETA UBAGUZI NAKUMALIZA


Mario Balotelli akiwa kwenye mazoezi na kikosi cha timu ya taifa ya Italia

Balotelli alipokuwa akitangaza azma ya kumtoa 'ngeu' mtu yeyote atakaemkebehi na kumdharau katika michuano ya Ulaya huko Poland na Ukraine

Mshambuliaji mtukutu wa Manchester City anayechezea timu ya taifa ya Italia, Mario Balotelli amesema kuwa ataondoka uwanjani endapo ataonyeshwa vitendo vya ubaguzi wa rangi wakati wa Fainali za Euro zinazoandaliwa kwa pamoja kati ya Poland na Ukraine.

Jarida ya Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, lilisema kuwa wenyeji wa Fainali za Euro wamekuwa na tabia ya ubaguzi wa rangi na UEFA imesisitiza kuwa m chezo unawez akuvunjwa endapo itatokea hali hiyo.

Mshambuliaji huyo wa Italia, Balo, 21, alisema: “Endapo mtu atanipiga kwa ndizi mtaani, ni wazi nitakwenda jela kwa sababu nitamuua.“Ubaguzi wa rangi hauna nafasi kwangu, siwezi kuuendekeza. Naamini hakutakuwa na matatizo katika Fainali za Euro, na ikitokea nitarudi nyumbani.

“Lakini tuko katika michuano ya Euro 2012, najua haiwezi kutokea.”


Balotelli, 21, alikumbana na hali hiyo akiwa na City katika michuano ya Ligi ya Europa walipocheza na Porto mapema Februari.Lakini hakupata tabu sana na alipokuwa Inter Milan mwaka 2009 aliwahi kurushiwa ndizi.

Balotelli aliiambia France Football: “Najua wanaweza kunifuata askari kuja kunikama, kwa sababu naapa, nna ninaapa kweli nitampa mtu kipigo cha sawasawa. Nitawapiga kweli. “Lakini bado nina imani hilo haliwezi kutokea.”

Tukio lingine lililotokea Italia ni wakati Balotelli alipodhihakiwa na mashabiki wa Juventus.


Alisema: “Nakumbuka vizuri na hiyo ni kwa sababu nafunga mabao. Kimsingi, watakuwa watu wazuri na hawawezi kufikiria hilo la kukufanya ukasirike. Kikubwa wanachofanya ni kukuchanganya kwa kukukebehi.
Nilijifanya sioni lolote lililotokea kwa sababu nilitaka kucheza mpira. Nilikuwa bado mdogo. Nilichokifanya ni kumwambia mwamuzi. Lakini kama ningemwambia mwamuzi asimamishe mchezo nisingefunga.”

No comments:

Post a Comment