Tuesday, May 22, 2012

MILOVAN ALAMBA DUME SIMBA SPORTS CLUB


Kocha Milovan(Kushoto) na mwenyekiti wa Simba(Kulia)Rage

Timu ya Simba Sport Club ambao ni mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara wamemuongezea mkataba kocha wao Milovan Cirkovic kwa miaka miwili zaidi na kumfanya kocha huyo kuwa na uhakika na "umatemate" zaidibaada ya ule waliokuwa wamempa mwanzo wa miezi sita kumalizika.
Mkataba uliomalizika wa Milovan ni baada ya kurithi mikoba ya Mganda Moses Basena, akitangaza kumuongezea mkataba huo kocha Milovan, Makamu mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange Kaburu amesema" Kipimo cha mafanikio ya kocha ni mataji na soka safi,kitu ambacho sisi kama viongozi wa Simba tumekishuhudia chini ya Profesa Milovan,sasa hatuoni kwanini tusimuongezee mkataba."
Kaburu aliongeza kuwa sababu nyingine ni mipango mizuri aliyonayo Milovan kwa soka la Vijana wa Simba, ni kitu ambacho hakipingiki katika ligi iliyokwisha tumeshuhudia Vijana wa Simba wakipata nafasi ya kucheza na dhahiri wameonesha uwezo wao,mfano mzuri Jonas Mkude,Singano na wengine yote hayo ni mafanikio ya kocha Milovan kuwapa nafasi Vijana kuonesha "udambwidambwi" wao.

No comments:

Post a Comment