Wednesday, May 9, 2012

OKWI, BOBAN NA SUNZU KWENYE REKODI ZA C.A.F ,SIMBA YAIFUATA AL AHLY SHANDY



Emmanuel Okwi

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Simba wanaondoka leo kwenda Khartoum, Sudan tayari kwa mchezo wa marudiono dhidi ya Al Ahly Shendi, washambuliaji nyota wa Wekundu hao wa Msimbazi, Emmanuel Okwi na Felix Sunzu wameingia kwenye rekodi ya wafungaji bora Afrika katika michuano ya Kombe la Shirikisho la soka Afrika.

Haruna Moshi "BOBAN"

Okwi, raia wa Uganda na Felix Sunzu ambaye ni Mzambia, wote wametajwa kuwa na mabao matatu kila mmoja kwa mujibu wa mtandao wa tensport.com.
Mshambuliaji huyo anayechezea pia Uganda Cranes, alifunga bao moja dhidi ya Entente Sportive de Setif katika mchezo wa kwanza kati ya mawili walioshinda mabao 2-0 Dar es Salaam na moja likifungwa na Haruna Moshi.

Felix Sunzu
Mchezo wa marudiano, Okwi alifunga moja wakati Simba ikilala mabao 3-1. Mshambuliaji huyo alifunga dhidi ya Al Ahly Shendi kati ya mabao matatu huku mengine yakifungwa na Boban na Patrick Mafisango.
Kwa hali hiyo, Boban na Sunzu kila mmoja wana mabao matatu. Sunzu aliyafunga katika mchezo walioshinda mabao 2-1 dhidi ya Kiyovu ya Rwanda na lingine likifungwa na Parick Mafisango.
Mbali na wachezaji hao, wengine wenye mabao matatu ni Komara, Niamba wote wa Leopards ya Congo, Chinyengetere (Hwange ya Zimbabwe, Moco (InterClube (Angola) na Raouf (ENPPI, Misri) na Seri wa Asec Mimosa ya Ivory Coast.
Mpaka sasa Fiston (Lydia Academic, Burundi) na Girma wa St George ya Ethiopia wana mabao manne kila mmoja.
Wakati huo huo, msafara wa Simba unaondoka leo mchana kwenda Sudan kupitia Nairobi, Kenya tayari kwa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy baada ya kukwama kuondoka kutokana na majambazi kuvunja na kuiba katika ubalozi wa Sudan.
Juzi usiku majambazi walivunja sefu ya kuhifadhia fedha na kuiba zaidi ya dola 40,000 ubalozini hapo pamoja fedha nyingine pamoja na kuiba kompyuta zote zinazotumika kuhifadhia kumbukumbu mbalimbali.
Kutokana na hali hiyo, Simba walikwama kupata viza zao juzi na jana na zinataraji kutolewa leo asubuhi kabla ya kuondoka saa 10:00 kwenda Sudan kupitia Nairobi ikiwa na wachezaji wote wa timu hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alithibitisha juzi kutokea tukio hilo.

No comments:

Post a Comment