Thursday, June 14, 2012

DI MATTEO NAMBA YA BAHATI YAFYATUKA SASA KOCHA MKUU CHELSEA


Kocha alielamba dume Chelsea Roberto Di Matteo

Chelsea hatimaye imemteua Roberto Di Matteo kama meneja wake wa kudumu kwa kutiliana saini mkataba wa miaka miwili na sasa Di Matteo ana uhakika na umatemate kama kocha mkuu kwa nyundo mbili.
Di Matteo aliwekwa kama kocha wa mda kufuatia kutimuliwa kwa Andre Villas-Boas mnamo mwezi Machi, na akaweza kuiongoza klabu hio akifanikiwa kuifikisha na kushinda fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na vilevile kombe la FA la England.


Di Matteo kulia akiteta jambo na kocha alietimuliwa Andre Villa Boas, ambae sasa Di Matteo ndie amerithi Mikoba yake.

Meneja huyo aliyekua kiongozi wa MK Dons na pia West Brom, Di Matteo alipoteza mechi tatu tu kati ya mechi 21 alizosimamia, na kutokana na hali hiyo wachezaji wengi wa klabu waliunga mkono ateuliwe kama meneja wa kudumu hususan baada ya kushinda kombe lililoikwepa klabu hio kwa mda mrefu la Mabingwa wa Ulaya.

Di Matteo akiwa ameshikilia ndoo ya Ubingwa wa Ulaya alipoiwezesha Chelsea kulinyakua hivi karibuni baada ya ukata wa kombe hilo kwa muda mrefu na kumhakikishia Di Matteo kuwa na uhakika wa umatemate kwa miaka miwili kama kocha mkuu





Cherekochereko asie na mwana aeleke jiwe Di Matteo juujuu baada ya kutwaa kombe la mabingwa wa Ulaya

No comments:

Post a Comment