Thursday, June 14, 2012

EURO 2012 GOMEZ APELEKA KILIO UHOLANZI IKILALA DORO MBELE YA UJERUMANI


Pepe akishangilia baada ya kuipatia Ureno kamba ya kwanza


Ureno imeiadhibu Denmark 3-2 katika mtanange wa kundi B katika michuano ya Euro 2012.
Ushindi wa Ureno wa 3-2 dhidi ya Denmark katika michuano wa Euro 2012 unaweka matumaini ya nchi hiyo kuendelea hadi robo fainali.
Bao lililonusuru matumaini hayo lilitiwa kimyani na Silvestre Varela aliyeletwa kipindi cha pili aliyefunga bao na kufuta bao la Nicklas Bendtner la kusawazisha mapema katika kipindi cha pili.


Varela alieingia kipindi cha pili akishangilia goli la tatu na la ushindi la Ureno baada ya kutupia kambani.

Ureno iliongoza kupitia kipindi cha kwanza kupitia wachezaji wasiotarajiwa ambapo beki Pepe na Helder Postiga waliipatia Ureno mabao ya kuwapa matumaini ya kupiga hatua.

Lakini kukosa fursa kadhaa kwa nyota wao Cristiano Ronaldo kulitishia kuiangusha Ureno na kurejea nyumbani mapema.


Christia Ronaldo akijaribu kumhadaa mlinzi wa Denmark lakini alikosa mabao lukuki katika mechi hiyo

Ushindi huu unaiweka Ureno sambamba na Denmark kwa pointi kutokana na ushindi wa Denmark dhidi ya Uholanzi katika mechi ya ufunguzi kwa pande hizo mbili.

Katika mchezo wa pili siku ya Jumatano, Mario Gomez wa Ujerumani aliwafunza wachezaji wa Uholanzi namna ya kufunga mabao, walipoondoka na ushindi wa magoli 2-1.


Gomez (23) akitupia kambani goli la kwanza la Ujerumani

Hapa hapatoshi!!! Robben akijaribu kufanya udambwidambwi katika mtanange huo

Mshambulizi huyo wa Bayern Munich kwa upesi aliweza kugeuka alipopokea mpira kutoka kwa Bastian Schweinsteiger na kuandikisha bao la kwanza la Ujerumani katika dakika ya 24, na baadaye kuongezea la pili katika dakika ya 38, katika kuhakikisha Uholanzi itaondoka katika michuano ya Euro 2012 mapema.


Robin Van Persie na Van Der Vaart wakishangilia goli la kufutia machozi lililotupiwa kambani na Van Persie

Robin van Persie, ambaye alishindwa kuitumia nafasi nzuri iliyojitokeza na kuiwezesha Uholanzi kuongoza kufunga, hatimaye aliwafungia bao la kujituliza, lakini timu yake ikashindwa kufunga magoli zaidi.
DENMARK  2-3  URENO


UJERUMANI  2-1  UHOLANZI

No comments:

Post a Comment