Wednesday, June 27, 2012

EURO 2012 NUSU FAINALI YA MAFUNDI WANAOJUANA SPAIN Vs URENO


Christiano Ronaldo wa Ureno(Real Madrid)

Xavi Alonso wa Uhispania (Real Madrid)

Miamba ya soka barani Ulaya Ureno na Uhispania leo zitapepetana katika nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Ulaya katika dimba la Donbass,Donetsk.
Timu hizo mbili zinakutana zikiwa zimesheheni nyota wanaocheza soka la hali ya juu huko barani Ulaya na kwa idadi kubwa ya wachezaji wanakipiga La Liga Uhispania katika timu za Real Madrid na Barcelona hakika leo hatumwi mtoto dukani.

Ureno itamtegemea zaidi Christiano Ronaldo na Beki matata Pepe, Varela,Moutinho,Meireles,Luis Nani na wengineo wengi. huku wapinzani wao Uhispania ikimtegemea zaidi A.Iniesta kama mchezeshaji na wakali wengine kama Xavi,Torres,Sergio Bosquets,Sergio Ramos,Gerald Pique,David Silva,Pedro,Fbregas na mlinda mlango mashuhuri Iker Casillas. 

Ureno wamefika hatua ya nusu fainali baada ya Kujikusanyia pointi 6 na kukamata nafasi ya pili katika kundi B. na hivyo kuingia katika hatua ya robo fainali ambapo walikutana na Ugiriki na kufanikiwa kuwasambaratisha wagiriki kwa bao moja kwa nunge likitiwa kambani na Christiano Ronaldo katika dakika ya 78.

Uhispania ilifanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali za michuano ya EURO 2012 pale ilipojikusanyia pointi 7 na kuibuka kidedea katika kundi C, katika hatua ya robo fainali hizo ilikutana na vigogo wengine wa Ulaya Ufaransa na bila aibu kuwafurumusha nje ya michuano hiyo kwa mabao 2 kwa buyu huku mabao yote yatupiwa kambani na Xavi Alonso katika dakika ya 18 na 90.

Katika mtanange wa Nusu fainali ya leo kati ya Ureno na Uhispania ni vigumu mno kutabiri nani ataibuka meno nje kwa jinsi vikosi vyote vilivyosheheni nyota wanaojuana mno kwa ukweli kuwa wanatoka katika vilabu ambavyo hukutana mara kwa mara katika ligi za Ulaya sana sana La Liga ya Uhispania na Premier league ya Uingereza.

Andre Iniesta wa Uhispania (Barcelona)

Gerard Pique Gerard Pique of Spain in action during the International Friendly between Spain and England at the Ramon Sanchez Pizjuan Stadium on February 11, 2009 in Seville, Spain.  (Photo by Alex Livesey/Getty Images) *** Local Caption *** Gerard Pique
Gerald Pique wa Uhispania (Barcelona)


Torres wa Uhispania (Chelsea)

Cesc Fabregas - Spain v Italy - Group C: UEFA EURO 2012
Fabregas wa Uhispania (Barcelona)


Xavi Hernandez (Barcelona)

Moutinho wa Ureno (Sporting Lisbon)


Pepe wa Ureno (Real Madrid)


Silvester Valera wa Ureno (FC Porto)


Luis Nani wa Ureno (Manchester United)

No comments:

Post a Comment