Wednesday, June 20, 2012

EURO 2012 ROONEY AWAFUNGASHIA VIRAGO WENYEJI


Rooney akichanja mbuga

Rooney akitupia kambani kwa kichwa goli pekee la Uingereza

Wayne Rooney alirejea dimbani akiwa shujaa wa timu ya England usiku wa Jumanne, baada ya kutokuwepo kwa muda kufuatia adhabu ya UEFA, na bao lake moja dhidi ya Ukraine liliiwezesha timu yake kukwea kileleni katika kundi D.


Kocha wa Uingereza Roy Hodgson akimpongeza Rooney kwa kazi nzuri

Vile vile bao hilo linamaanisha England imeweza kuiepuka Uhispania katika robo fainali, na sasa itacheza dhidi ya Italia.
Rooney, akiwa karibu sana na kipa wa Ukraine, Andriy Pyatov, aliweza kufunga kwa kichwa, mpira uliokuwa wa majaro ya juu kwa juu kutoka kwa nahodha Steven Gerrard.

Licha ya England kuibuka washindi, Ukraine walifanya juhudi kubwa na kupata nafasi nyingi zaidi za kusawazisha, lakini yote hayo hayakufua dafu.

Ukraine walistahili kupata bao wakati mkwaju wa Marko Devic ilikuwa wazi umevuka mstari, lakini kufuatia juhudi za John Terry katika kuondosha mpira huo, pengine mwamuzi alishawishika kwamba kweli mpira haukuvuka msitari.

Ushindi wa Sweden wa magoli 2-0 dhidi ya Ufaransa ulihakikisha kwamba England wanafuzu kuingia robo fainali kama timu iliyoongoza katika kundi D.

Mlinzi wa Uingereza Lescott akichuana vikali na Shevchenko wa Ukraine

Mtifuano kati ya Kacheridi na Welbeck


Tulia weweee, daruga kali la Oleg Husev limemuangukia Ashley Cole

Ukraine  0-1  England

No comments:

Post a Comment