Wednesday, June 20, 2012

UFARANSA YACHAPWA NA SWEDEN LAKINI YATINGA ROBO FAINALI EURO 2012 USO KWA USO NA SPAIN

French Goalkeeper Hugo Lloris Dives AFP/Getty Images
Mlinda mlango wa Ufaransa Hugo Lloris akichupa bila mafanikio

Bao lililotupiwa kammbani kwa ustadi na Zlatan Ibrahimovic limeisaidia Sweden kuichapa Ufaransa magoli 2-0 katika mechi ya kundi D usiku wa Jumanne, na kuhakikisha wameisukuma Ufaransa katika nafasi ya pili katika kundi, na pia kuilazimisha kukutana na mabingwa watetezi Uhispania katika mechi ya robo fainali ya Euro 2012.

Sweden v France - Group D: UEFA EURO 2012
Swedish Supporters AFP/Getty Images
Wachezaji wa Sweden Wakishangilia ushindi baada ya kuiangushia kichapo Ufaransa

Ufaransa walizidiwa katika mechi hiyo, na Ola Toivonen al-manusra aipatie Sweden bao la kwanza baada ya kuachia nduki iliyogonga sehemu ya nje ya mwamba wa goli.
Hatimaye Ibrahimovic alipata bao kupitia nduki kali kutoka umbali wa yadi 15, baada ya kupenyezewa pande maridadi na Sebastian Larsson.

Olivier Giroud alitupia kwa kichwa na kuiwezesha Sweden kupata bao lao la pili.

Kichapo cha Ufaransa kina maanisha hatua yao ya kucheza pasipo kushindwa katika msururu wa mechi 23 zilizopita tangu waliposhindwa wakiwa nyumbani na Belarus mwezi Septemba mwaka 2010 imesitishwa.

French Forward Karim Benzema (C) And French Defender Adil Rami React At The End Of The Euro 2012 Football  AFP/Getty Images
wachezaji wa Ufaransa hawaamini kilichotokea
 (L-R) Adil Rami, Mathieu Debuchy, Philippe Mexes And Alou Diarra Of France Look Dejected  Getty Images
Adil Rami,Mathieu Debuchy,Phillipe Mexes na Alou Diarra wameloa kwa kichapo


Huo ndio muda mrefu zaidi ulioandikishwa timu kucheza pasipo kushindwa kwa upande wa mechi za kimataifa.

Ufaransa wameshindwa baada ya mechi 24 za kimataifa, na kocha Laurent Blant sio tu atakuwa na wasiwasi katika kupambana na mabingwa wa Ulaya na wa dunia pia, bali pia kuhusiana na timu yake kucheza mchezo wa kiwango duni.

Sweden tayari walikuwa wameondolewa katika mashindano baada ya kushindwa katika mechi zao mbili za mwanzo, lakini nia yao ilikuwa ni kucheza kadri ya uwezo wao kabla ya kurudi nyumbani.

Jumapili iliyopita, wachezaji hao walikataa ushauri wa meneja Erik Hamren wa kupumzika, na badala yake waliamua kuitumia siku hiyo katika kufanya mazoezi zaidi.

No comments:

Post a Comment