Monday, June 11, 2012

ITALIA NA HISPANIA ZAGAWANA UMASKINI KWA SARE YA 1-1


De Natale akitupia kambani mbele ya Iker Casilas

Mabingwa wa Dunia Uhispania wameanza utetezi wa Kombe lao la ubingwa wa mashindano ya Ulaya kwa sare ya 1-1 dhidi ya Italia katika pambano la kundi C mjini Gdansk.


Barwuah Balloteli akioneshana kazi na Pique

Italia ndiyo iliyotangulia baada ya kipindi cha kwanza kumalizika bila bao lolote kufungwa na alikua Antonio Di Natale aliyeingia badala ya Balloteli kufunga bao katika dakika ya 60.


Mwachemwache za mashabiki wa Italia

Dakika nne baadaye Mabingwa wa Dunia na Ulaya walifumania lango la Italia na licha ya juhudi na umahiri wa Mabeki David Silva alimuona Cesc Fabregas na kumuwekea pasi maridhawa na bila kufanya makosa akaupenyeza mpira kumpita goli wa Italia Buffon.


Fabregas akiiandikia Hispania bao la kuongoza

Matokeo hayo yanaliweka kundi la C wazi ambapo Italia na Uhispania zinaondoka zote zikiwa na pointi moja.
Kabla ya mashindano haya wadadisi walionelea kama Uhispania itakabiliwa na kibarua kigumu kutetea taji lake kutokana na wachezaji wake wengi kuwa wachofu mno. Jumla ya wachezaji 23 wa timu hii ya Taifa wamecheza jumla ya dakika 89,884 katika msimu uliopita ikilinganishwa na wenzao walioshiriki kwa upungufu wa dakika 17,000.


Walinda milango Iker Casillas wa Hispania na Buffon wa Italia wakipeana pongezi kwa kupangua michomo mikali katika mtifuano wa timu zao

Timu mbili zilizomo kwenye kundi la C Jamhuri ya Ireland na Croatia lazima zimeridhishwa na matokeo haya zikiona kua na fursa ya kufanya vyema na uwezekano mkubwa wa kufuzu kutoka michuano ya makundi.
Hispania Vs Italia

No comments:

Post a Comment