Monday, June 11, 2012

EURO 2012,CROATIA YAIDUNGUA JAMHURI YA IRELAND


Goooooooooo, bao la kwanza la Croatia

Goli la pili la Croatia...kazi imeanza!!

Matumaini ya Jamhuri ya Ireland kuvuka hatua ya makundi katika mashindano ya Euro 2012 yalididimia, baada ya kulazwa magoli 3-1 na Croatia katika mji wa Poznan, Poland.
Mario Mandzukic aliweza kufunga kwa kichwa, huku juhudi za kipa Shay Given kuuzia mpira huo zikikosa kufua dafu.
Lakini juhudi za wachezaji wa Jamhuri ya Ireland hatimaye zilifanikiwa, wakati Sean St Ledger aliposawazisha.

Ireland wakisawazisha bao na kuwa 1-1 kabla ya dhahama kuwaangukia


Shabiki wa Jamhuri ya Ireland akiwa katika swaga za aina yake

Hata hivyo, kabla kipenge cha kukamilisha nusu ya kwanza ya mchezo, Nikica Jelavic alibadilisha matokeo, na kuiwezesha Croatia kuongoza 2-1.

Mandzukic aliweza kuandikisha bao la tatu, ambalo mpira uliingia wavuni ukisindikizwa kimakosa na kipa wa Given.

Jamhuri ya Ireland haiwezi kulalamika sana kuhusiana na matokeo ya mechi hiyo, kwani ilikuwa wazi timu yao bado haijajiandaa vyema.

Kabla ya mechi, mashabiki wengi kutoka Jamhuri ya Ireland walikuwa na matumaini ya kufanya vyema katika mechi hiyo ya kundi C, lakini uwanjani ilikuwa ni wazi kwamba Croatia ndio timu bora, meneja wao mzoefu, Giovanni Trapattoni, bila shaka itambidi kufanya kazi ya ziada ikiwa Jamhuri ya Ireland itaepuka fedheha katika mashindano hayo.
Croatia vs Ireland

No comments:

Post a Comment