Monday, June 11, 2012

STARS YAWALIZA GAMBIA,SAMATTA KAMA KAWA


Mshambuliaji wa Star Mbwana Samatta"Samagoal" akipiga kichwa langoni mwa Gambia

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars jana iliwatoa kimasomaso watanzania baada ya kuibugiza Gambia kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba kuu la taifa jijini Dar es salaam.Gambia ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji Mustafa Jarju akitupia kambani kwa kichwa.
Wakati Gambia wakiamini wataiadhiri Stars nyumbani hamad...Shomari Kapombe akazifuta ndoto za wagambia kwa kusawazisha goli maridadi akitupia kambani kwa kichwa na kufanya matokeo kuwa 1-1 dakika ya 65 ya mtanange huo.

Mbwana Samatta"Samagoal" kama wanavyomuita mashabiki wa TP Mazembe ya kule jamhuri ya kidemokrasia ya kongo anakokipiga alikuwa mwiba mkali katika mechi hiyo kwa udambwidambwi wake kama kawa akaipepeta ngome ya Gambia kwa kumuadhiri beki wa kushoto kwa vyenga vya maudhi na kumuacha chini,Samatta alimimina krosi maridadi langoni katika mwachemwache ndipo beki wa Gambia akaunawa mpira katika eneo la hatari na mwamuzi bila ajizi akatenga maguu kumi na mbili ya mtu mzima..kama analia Erasto Nyoni akatupia kamba ya pili kwa Stars na ndipo hekaheka ,nderemo,mwachemwache zilipoibuka katika dimba kuu la Taifa..mpaka mwisho wa Mchezo Stars 2-1 Gambia. na Stars imejiweka pazuri katika kampeni za kuwania kushiriki kombe la dunia nchini Brazil 2014.

Kikosi cha Stars

Kikosi cha Gambia


Mbwana Samatta akiwa amewekwa chini baada ya kutaka kuleta madhara langini mwa Gambia


Nyinyi watoto wadogo tuu!!! 


Mwachemwache kati ya Samatta na mabeki wa Gambia


Kambaaaaaaa!! Erasto Nyoni akishangilia pamoja na Samatta baada ya Nyoni kutupia kamba ya pili na ya ushindi ya Stars


Ndio ukubwa kakaa..Ndivyo anavyosema kocha wa Stars Kim Poulsen akimwambia kocha wa Gambia Luciano Mancini baada ya mtanange kumalizika kwa Star kuibuka washindi



No comments:

Post a Comment