Tuesday, June 26, 2012

VENUS WILLIAM AONDOLEWA MAPEMA WIMBLEDON


Venus akirudisha mchomo kwa mpinzani wake Elena Vesnina

Bingwa mara tano katika mashindano ya tennis ya Wimbledon, Mmarekani Venus Williams, amesema hana nia ya kuachana na mchezo huo baada ya kuondolewa katika siku ya kwanza ya mashindano ya mwaka 2012 ya Wimbledon, katika raundi ya kwanza, alipopokea kipigo kitakatifu kutoka kwa mchezaji Mrusi, Elena Vesnina.
Venus, mwenye umri wa miaka 32, na anayeugua ugonjwa unaofahamika kama Sjogren's Syndrome, alishindwa 6-1 6-3 siku ya Jumatatu.
Mpinzani wake Vesnina amepangwa katika nafasi ya 79 katika orodha ya wachezaji bora zaidi wa tennis wa kike ulimwenguni.

Kiboko ya Venus Williams,Elena Vesnina akipeleka mchomo kwa Venus

"Haiwezekani nipumzike tu na kukata tamaa," alielezea Williams.

"Sina muda wa kujisikitikia. Hilo sio jambo zuri. Nitautumia muda wangu katika mawazo yanayonipa nguvu. Ninaupenda mchezo huu."

Mara ya kwanza Williams kushindwa katika raundi ya kwanza ilitokea mwaka 1997, wakati alipoingia pambano lake la kwanza la Wimbledon, na wakati huo alikuwa hata hayumo miongoni mwa wale waliopangwa katika mashindano hayo kama wachezaji bora.

Ni wanawake wawili tu ulimwenguni ambao wameshawahi kupata ubingwa wa Wimbledon mara nyingi kumshinda Williams, lakini tangu mwaka 2008, hajawahi kuibuka bingwa wa mashindano hayo.

Mara tu baada ya ushindi wake wa mwisho, iligunduliwa kwamba anaugua ugonjwa wa Sjogren's Syndrome, na ambao humfanya mgonjwa kujihisi ni mchovu mno, na katika sehemu mifupa inaungana, maumivu.

Ayaaaaaaaa nimechapwa!!!!!


Kudadekii leo Venus hutoki hapa!!

Venus Williams baada ya kupokea kichapo kitakatifu kutoka kwa Mrusi Elena Vesnina


No comments:

Post a Comment