Friday, June 8, 2012

WAJUE NYOTA WA AFRIKA WATAKAOKIPIGA EURO 2012



Kiungo hodari Yann M'Vila atachezea timu ya Ufaransa na amekuwa akikipiga tangu enzi za kocha Laurent Blanc alipoanza kuinoa Ufaransa mwaka 2010.


Mshambuliaji wa Timu ya Manchester United Danny Welbeck atakipiga England na alitia kambani bao lake la kwanza dhidi ya timu ya Ubelgiji wakati wa mechi ya kirafiki kwa maandalizi ya kombe la Euro 2012 mapema mwezi huu. Alianza kukipiga England mwaka 2011 dhidi ya Ghana,nchi ambayo ilijaribu kumshawishi kuichezea kwa sababu ya mizizi yake ambayo iko nchini humo.


Wachezaji kadhaa watakaokipiga katika michuano hii ya Euro, huenda waliwahi kuwakilisha nchi zao za Afrika . Miongoni mwa wachezaji wazaliwa wa Afrika ni mlinzi wa Ufaransa Steve Mandanda mzaliwa wa Kinshasa , mji mkuu wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Mcheza kiungo wa kati Sami Khedira amecheza katika mechi 20 akikipiga na  mabingwa wa ligi ya Uhispania, Real Madrid na anatarajiwa kuwa nyota wa Ujerumani kama ilivyokuwa katika michuano ya kombe la dunia miaka miwili iliyopita. Hata hivyo Khedira mwenye umri wa miaka 25, alizaliwa Tunisia.


Mshambuliaji wa Manchester United Patrice Evra ni nahodha wa zamani wa timu ya Ufaransa aliyezaliwa mjini Dakar (Senegal) kabla kuhamia nchini Ufaransa na babake aliyekuwa balozi. Evra mwenye umri wa miaka 30, ana hamu ya kuonyesha cheche zake.


Mchezaji mwingine wa Manchester United, Nani atakaekipiga na nchi ya Ureno, angeweza kuchezea timu ya nyumbani kwao kisiwani Cape Verde. Mshambuliaji huyo wa pembenei mwenye umri wa miaka, 25, aliishi kisiwani humo utotoni mwake kabla ya kuhamia mjini Lisbon, Ureno.


Licha ya kukaa msimu wote kwenye benchi la magwiji wa soka nchini Uhispania, Barcelona, Ibrahim Afellay atakipiga na timu ya Uholanzi kwenye michuano hii. Ibrahim angekipiga Morocco kwani ndiko alikozaliwa, na ambako wazazi wake wana mizizi yao lakini aliamua kuwakilisha nchi yake miaka mitaano iliyopita wakati alipocheza kwenye dimba la kombe la dunia mwaka 2010 World.

 
Angelo Ogbonna beki wa kilabu ya Torino atachezea Italia, lakini bila shaka angechezea Nigeria ambako wazazi wake wanatoka.





Adil Rami (kulia) wa Ufaransa atacheza kwenye timu ya Ufaransa akiwa na Ogbonna kama beki. Akiwa na umri wa miaka 26, mlinzi wa kilabu ya Valencia alikataa fursa ya kuchezea Morocco, ambako wazazi wake wanatoka kabla ya kuchezea kilabu ya Laurent Blanc ya Norway katika mechi ya kirafiki kabla ya kombe la dunia mwaka 2010. Rami alicheza mechi tisa kati ya kumi za kufuzu kwa kombe la Euro mwaka huu.


Theodor Gebre Selassie atachezea jamuhuri ya Czech na yeye ni mzaliwa wa Ethiopia. Mlinzi huyo alichezea Czech katika mechi zao za kufuzu kuwania kombe hilo, ikiwemo mechi waliyoshinda dhidi ya Montenegro.


Mshambuliaji matata wa Manchester City, Mario Balotelli, ameamua kuonyesha heshima kwa Ghana alikozaliwa, kwa kuandika majina yake yote ya Ghana na Italia kwenye jezi yake atakayochezea katika michuano hiyo ya Euro 'Barwuah Balotelli' . Alizaliwa mjini Palermo kwa wazazi wake wa Ghana ambao jamaa zao wanaishi eneo la Brong Ahafo nchini Ghana ingawa aliasiliwa na familia ya kitaliano.

Karim Benzema Karim Benzema of France in action during the international friendly match between England and France at Wembley Stadium on November 17, 2010 in London, England.
Karim Benzema atakipiga na timu ya taifa ya Ufaransa ili hali yeye ni mzaliwa wa Algeria







Jerome Boateng atakipiga na timu ya taifa ya Ujerumani ili hali ni mzaliwa wa Ghana


Jores Okore atakipiga na timu ya taifa ya Denmark lakini yeye ni mzaliwa wa Ivory Coast

Khalid Boulahrouz atakipiga na timu ya taifa ya Uholanzi na yeye ni mzaliwa wa Morocco.

Blaise Matuidi atakuwa akikipiga na Ufaranca ili hali yeye ni mzaliwa wa Angola.


Samir Nasri kiungo mshambuliaji wa Man City atakuwa akikipiga na timu ya taifa ya Ufaranca lakini Nasri ni mwenye asili ya Algeria.

Alou Diarra ni mchezaji mwenye asili ya Mali lakini katika michuano ya EURO 2012 anakipiga na timu ya taifa ya Ufaransa.

Hatem Ben Arfa ni mchezaji wa Newcastle United ya Uingereza atakipiga na Ufaransa lakini yeye ni mzaliwa wa Tunisia.

Rolando mchezaji wa FC Porto ya Ureno atakaekipiga na timu ya taifa ya Ureno lakini yeye ni mzaliwa wa visiwa vya Cape Verde.

No comments:

Post a Comment