Tuesday, July 10, 2012

KEITA AONDOKA BARCELONA NA "NDOO"14 HUKU TITO AKIMRITHI PEP GUARDIOLA


Seydou Keita

kiungo wa Mali Seydou Keita amekihama klabu ya Barcelona baada ya kukipiga kwa miaka minne.
Katika muda huo wa miaka minne, Keita aliisaidia Barcelona kuzoa jumla ya vikombe 14.
Wakati wakithibitisha kuondoka kwa mwamba huyo, Barca walimshukuru Seydou Keita kwa juhudi zake za kuiletea klabu hiyo ya Uhispania mafanikio na vile vile wakamtakia kila lakheri anakokwenda.

Keita na Sanchez wakiwa wamebeba kombe wakikipiga Barcelona

Kwa wakati huu kuna fununu kwamba mchezaji huyo wa Mali huenda anahamia klabu moja ya Uchina, Dalian Aerbin
Ikiwa hatiamae ataishia China basi Keita hatakuwa mchezaji wa kwanza kutoka bara la Afrika kufanya hivyo.
Majuzi nahodha wa timu ya Ivory Coast Didier Drogba aliwafuata Frederic Kanoute na Yakubu Aiyegbeni wa Nigeria kujiunga na timu za ligi kuu ya China.
Keita, mwenye umri wa 32, alijiunga na Barcelona mwaka 2008 kutoka Sevilla akiwa ni mchezaji wa kwanza kabisa ambaye Pep Guardiola alimsajili mara tu alipokwaa uongozi wa Barca.
Kabla ya hapo mchezaji huyo alikuwa Olympic Marseille, Lorient na Lens zote za Ufaransa na ndio baadaye akahima Seville ya Uhispania.
Keita amehama baada ya Guardiola kuondoka kama Meneja wa Barcelona na mahali pake kuchukuliwa na aliyekuwa naibu wake Tito Vilanova

Tito Vilanova kocha alierithi mikoba ya Pep Guardiola


Tito Vilanova akiwa na Pep Guardiola

No comments:

Post a Comment