Tuesday, July 10, 2012

MPAMBANO WA SOKA WABUNGE WA SIMBA NA YANGA KATIKA PICHA


Timu za wabunge wa Simba na Yanga wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya mpambano

Waamuzi wa mpambano huo wakipiga picha ya pamoja na manahodha wa timu zote mbili

Wabunge wa Simba katika Dua kabla ya mtanange kuanza


Wabunge wa Yanga nao wakipiga dua kabla ya mtanange kurindima

Mashabiki wakiwahi mpambano

Mtanange umeanza


Mwamuzi wa mtanange huo Athuman Kazi akifuatilia kwa karibu kuhakikisha haki inatendeka


Mh Zitto Kabwe wa Simba akitoa pasi murua kama Iniesta vile!


Mbunge wa Simba akitiririka na kabumbu















Katibu uenezi wa CCM Nape Nnauye akifuatilia mpambano wa Wabunge wa Simba na wale wa Yanga katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es salaam


Benchi la ufundi la Wabunge wa Simba wakifuatilia mpambano


Benchi la ufundi la Wabunge wa Yanga wakiongozwa na kocha mkuu mpya wa Yanga


Mbunge wa Yanga akiwa hoi bin taaban


Mbunge wa Yanga akijaribu kuihadaa ngome ya wabunge wa Simba


Hali tete mlinda mlango wa wabunge wa Yanga baada ya kichapo kwa njia ya matuta 3-2


Wera weraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!! wabunge wa Simba hatimae waliwachapa wa Yanga katika matuta baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 0-0




Nani kama Simbaaaa woyooooo woyooooooooo


Hakunagaa zaidi ya Simba hakunagaa, hakunaaa hakunaaaa hakunaaaaaaaaaa!!!


Weraaaaa tupishe tupiteeee, tupisheeeee tupishe tupiteeeeeeee..Wabunge wa Simba wakiongozwa na Mh Zitto Kabwe na William Ngeleja kuserebuka baada ya kuwaangushia kisago wenzao wa Yanga kwa mikwaju ya penati 3-2
Mpambano Wabunge SIMBA Vs YANGA

Katika mtanange huo baada ya dakika 90 na kipyenga cha mwamuzi Athumani kazi kupulizwa matokeo yalikuwa ni 0-0. Mpambano huo wa kufurahisha na kusisimua uliopigwa katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni katika mchezo wa hisani kukusanya pesa kuchangia ujenzi wa mabweni kwa shule za sekondari nchini!

shukrani za pekee kwa waandaaji wa tamasha hilo ambalo pia liliwakutanisha wasanii wa Bongo flava na Bongo Movie hali kadhalika mpambano wa Masumbwi kati ya wasanii maarufu nchini na wenye kutengeneza vichwa vya habari katika redio na magazeti mbalimbali hapa nchini, ni Wema Sepetu na Jaquiline Wolper ambapo katika mpambano mpambano huo uliodumu kwa raundi mbili matokeo yalikuwa ni droo hakukuwa na mshindi.

No comments:

Post a Comment