Monday, August 27, 2012

DIAMOND AMSHIRIKISHA J MARTINS KWENYE SONG JIPYA


Naseeb Abdul "DIAMOND"

J Martins

Baada ya kufanya makamuzi ya nguvu kwenye shoo ya Big Brother Africa nchini Afrika ya Kusini, Diamond alianza kupata mialiko mbalimbali kutoka kwa wasanii wakubwa barani Afrika, na hivi sasa anatarajia kukamilisha kolabo yake anayoifanya na mwanamuziki kutoka Nigeria J Martin.

Kwa mujibu wa Diamond hivi sasa amesharekodi sehemu zake kwenye wimbo huo katika studio za MJ Records chini ya Prodyuza Marko Chali.

"Ingawaje nipo katika mchakato wa kusafiri kuelekea Marekani, lakini tayari nimeshaingiza voko za kazi yangu kwa Marco Chali na punde kolabo hiyo itaiva kama ilivyopikwa katika chungu safi.

"Chorus ya wimbo huo nimeimba mimi na mcheza shoo wangu Mose Iyobo"
anasema Diamond ambaye ameamua kumpa shavu dansa wake kutokana na kuonyesha uwezo mzuri katika kuimba.

J Martin ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani akichukua kozi maalum ya miezi mitatu ya masuala ya utayarishaji, tayari anausubiri wimbo huo ili aingize sauti yake.

Katika safari hii Diamond anakwenda na madansa wake wote wanne na msemaji wake. Diamond atafanya shoo katika mkutano mkubwa unaofanyika Marekani ambao wahudhuriaji wamemtaka akawape burudani.

No comments:

Post a Comment