Wednesday, September 19, 2012

ARSENAL YAIADHIBU MONTPELLIER

Arsenal imeanza vyema michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi baada ya kuichabanga Montpellier kwa magoli 2-1 nyumbani kwao katika dimba la La Mosson.

Wenyeji ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za wageni kwa bao maridadi la mkwaju wa penati iliyopigwa na Belhanda katika dakika ya 8 ya mchezo.
Watoto wa London,Arsenal "The Gunners" waliibuka kama mbogo aliejeruhiwa na kusawazisha goli katika dakika ya 15 likitupiwa kambani na Lucas Podolski.

Mtanange uliendelea huku kila timu ikisaka bao la ushindi na kuthibitisha hilo karata zilichezeka vizuri upande wa Arsenal na katika dakika ya 17 Gervinho aliwainua vitini mashabiki wa Arsenal kwa kutupia kambani goli la pili.

Mpaka mapumziko ngoma ilinoga kwa Arsenal kuwa mbele kwa kamba 2 kwa 1 ya Montpellier.Kipindi cha pili hakikuwa na mabadiliko ya matokeo ya mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wapatao 30,000 katika dimba hilo la Montpellier, na mpaka kipyenga cha mwamuzi kinaenda hewani matokeo yalikuwa Montpellier 1-2 Arsenal.

Podolski akitupia kambani goli la kusawazisha



Podolski akishangilia goli la kwanza

Hapa huendi kokote we mirasta!!!

Gibbs akijaribu kupiga majaro langoni mwa Montpellier


Gervinho akitupia kambani goli la pili

Gervinho - Montpellier Herault SC v Arsenal FC - UEFA Champions League
Gervinho akishangilia goli

Montpellier 1-2 Arsenal

No comments:

Post a Comment