Wednesday, September 19, 2012

REAL MADRID YAICHAPA MAN CITY KWA TAABU

Vicent Company akijaribu kumzuia Christian Ronaldo asilete maafa
 
Kamba ya  Cristiano Ronaldo katika dakika ya mwisho ya mchezo iliiwezesha klabu ya Real Madrid kuibangua Manchester City magoli 3-2 walipowakaribisha katika uwanja wao wa Bernabeu nchini Uhispania, mechi ya klabu bingwa barani Ulaya.

Kipa Joe Hart alikuwa mwiba kwa Real Madrid na aliiwezesha Man City kuendelea vyema bila kufungana mabao katika mechi ya Jumanne usiku, hadi Edin Dzeko alipowashangaza wenyeji kwa kupata bao katika kipindi cha pili.

Marcelo alisawazisha, kupitia mpira ambao ulimgusa mchezaji wa City kabla ya kubadilisha mwendo, lakini City wakafanikiwa kuendelea tena kuongoza baada ya mkwaju wa free-kick kutoka kwa Aleksandar Kolarov, wakati mpira moja kwa moja ulielekea hadi wavuni.
Kisha Karim Benzema aliweza kusawazisha, kabla ya Ronaldo kuandikisha bao la tatu na la ushindi katika mechi hiyo, na matokeo yakawa 3-2.

Kati ya mechi nyingine za klabu bingwa barani Ulaya ilikuwa ni pamoja na mchezo wa Arsenal, ambayo ilianza kampeni yake ya 15 ya mashindano hayo kwa kuwashinda wageni katika michuano hiyo, Montpellier ya Ufaransa.

Timu ya Arsene Wenger ililemewa ugenini baada ya dakika tisa, wakati nahodha Thomas Vermaelen aliposababisha penalti,ambayo ilifungwa na Belhanda, lakini kutokana na magoli mawili ya Arsenal kupatikana kwa haraka katika kipindi cha kwanza, kutoka kwa Lukas Podolski na Gervinho, hali ya mchezo ilibadilika, na Arsenal ikapata ushindi wa magoli 2-1.

Ushindi huo unamaanisha Arsenal na Schalke ya Ujerumani ndio vilabu ambavyo vinaongoza katika kundi B.

Shughuli pevu...Khedira na Kolarov

Yaya Toure akipasua mawimbi huku Essien akimfuatilia kwa karibu zaidi


Tevez chini ya ulinzi mkali


Edwin Dzeko akishangilia bao la pili



Mourinho na Ronaldo wakishangilia goli la tatu na la ushindi lililofungwa na Christiano Ronaldo kwa staili ya kufanana.


Ndio mpira kaka "FAIR PLAY" Mancini na Mourinho wakisalimiana kabla ya mpambano kuanza

REAL MADRID 3-2 MAN CITY

No comments:

Post a Comment